MKURUGENZI UPELELEZI MAKOSA YA JINAI HOI KITANDANI AGA KHAN...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/mkurugenzi-upelelezi-makosa-ya-jinai.html
Robert Manumba. |
Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, Dk Jaffer Dharsee alisema hospitalini hapo jana, kuwa hali ya afya ya Manumba bado inaangaliwa kwa karibu na madaktari.
Alisema Manumba anasumbuliwa na malaria kali iliyosababisha figo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Alisema kabla ya kuhamishiwa hospitalini hapo siku tatu zilizopita, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo vipimo vya awali vilichukuliwa.
Mwandishi alishuhudia jana Rais Jakaya Kikwete akiingia hospitalini Aga Khan kumjulia hali na baadaye alitoka bila kuzungumza kitu.
Kabla ya Rais Kikwete, mkewe Mama Salma naye alifika kumjulia hali mgonjwa na kuondoka.