MWANAMKE MWINGINE ABAKWA NA WAHUNI SITA NDANI YA BASI...

Basi hilo lilipofika maeneo haya ndipo tukio la ubakaji likatekelezwa dhidi ya mwanamke huyo.
Wanaume sita wamekamatwa kwa kumbaka mwanamke ndani ya basi kaskazini mwa India katika shambulio ambalo limetonesha kidonda cha tukio la kubakwa na kuuawa kwa mwanafunzi katika basi mjini New Delhi wiki kadhaa zilizopita.
Mwathirika alikuwa akisafiri kwenda nyumbani kwa wakwe zake mjini Punjab Ijumaa iliyopita ndipo anapodaiwa kunyakuliwa na kupelekwa wilaya ya mpakani mwa Amritsar, mji mtakatifu wa Sikh.
Wanaume watano wameungana na dereva na kondakta, ambao walimpakia kwenye pikipiki kuelekea kusikojulikana, na kuanza kumbaka mwanamke huyo wa miaka 29.
Walimtelekeza karibu na kijiji cha wakwe zake asubuhi iliyofuata ambapo aliwaeleza jamaa kuhusu mkasa mzima uliompata, polisi walisema.
"Wanaume sita wamekamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 29 ... baada ya kumchukua kwa nguvu hadi mafichoni usiku wa Januari 11," ofisa wa polisi Raj Jeet Singh alisema.
Mtuhumiwa wa saba bado anatafutwa na polisi, aliongeza.
"Mwanamke huyo, baada ya kuwa ametekwa, alibakwa vibaya usiku mzima na wanaume saba wanaotuhumiwa," alisema.
"Baada ya kumbaka mwathirika huyo usiku mzima, mmoja wa watuhumiwa alimtelekeza jirani na nyumba ya wakwe zake asubuhi ya kesho yake ambapo alisimulia mkasa mzima kwa wifi zake wawili."
Alipoulizwa kwanini hakubisha wakati alipopakizwa katika pikipiki kuelekea sehemu ambapo alishambuliwa, Singh alisema alikuwa 'na udhaifu kidogo kiakili', gazeti la The Indian Express limeripoti.
Ukubwa wa madhara aliyopata mwathirika huyo kutokana na majeraha bado hayajatangazwa, lakini uchunguzi wa awali umethibitisha kwamba alikuwa amebakwa, gazeti la Deccan Chronicle limeripoti.
Vyombo mbalimbali vya habari vya India vimeripoti kwamba watuhumiwa hao wamekiri wakati wa mahojiano ya awali.
Shambulio hilo limechukiza wengi sawa na lile la Desemba 16 ambapo kundi la wanaume lilimbaka na kumuua mwanafunzi mwenye miaka 21 mjini Delhi, ambapo wanaume watano wamepandishwa kizimbani katika kesi ambayo imechochea hasira katika nchi nzima ya India kufuatia vitendo alivyofanyiwa mwanamke huyo.
Partap Singh Bajwa, mwanasiasa wa chama cha Congress, ameshutumu polisi kwa kushinda kufanya ukaguzi wa nguvu kwenye mabasi yanayofanya safari zake katika jimbo hilo.
"Yote haya yanatokea kutokana na uzembe wa polisi ambao hawajisumbui kukagua mabasi yanayosafiri kwenye barabara kuu za nchini wakati wa majira ya usiku," Bajwa aliieleza AFP.
Waandamanaji kote India wametaka polisi kuwa macho na imara kushughulikia vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake, baada ya taarifa zilizoibuliwa katika shambulio hilo la mjini New Delhi.
Polisi na waendesha mashitaka wameshaelezea jinsi watuhumiwa wa ubakaji walivyomchukua mwanamke huyo na rafiki yake wa kiume katika basi la shule ambapo walipanda kwa raha zao baada ya kuwa wamekunywa pombe kwa kiasi kikubwa.
Basi hilo lilipita vituo kadhaa za ukaguzi wa polisi wakati huo wa usiku lakini hakuna hata sehemu moja basi hilo lilisimamishwa na maofisa wa polisi.
Baada ya kutokea malumbano na rafiki wa mwanamke huyo, kundi hilo linadaiwa kumpiga na kumbaka mwathirika huyo nyuma ya basi wakati likiendelea na safari kuzunguka Delhi kwa takribani dakika 45.
Pia walimdhalilisha kijinsia kwa kumshindilia kipande cha nondo sehemu za siri na kumsababishia majeraha makubwa ndani ya mwili wake kabla ya kumtupa nje ya basi.
Alifariki katika hospitali moja nchini Singapore ikiwa ni siku 13 baada ya shambulio hilo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item