WASHARIKA KANISA LA KKKT WAAZIMIA KUZUIA SADAKA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/washarika-kanisa-la-kkkt-waazimia.html
Halmashauri Kuu ya Usharika wa Ngateu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, imeazimia kuzuia sadaka zinazotakiwa kupelekwa Dayosisi kila wiki.
Azimio hilo lilifikiwa katika kikao cha wajumbe wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana ndani ya Kanisa la Usharika huo ambacho kilihudhuriwa pia na wajumbe wa Halmashauri Kuu za sharika nyingine 11 za Jimbo la Arusha Magharibi.
Akizungumza jana, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema usharika huo umeazimia kuwa sadaka za kuanzia jana hazitapelekwa Dayosisi kama ilivyo katika utaratibu wa uendeshaji wa kanisa hilo.
Kwa mujibu wa utaratibu huo, kila usharika katika makusanyo ya sadaka kila Jumapili na katika shughuli za katikati ya wiki, wanapaswa kupeleka katika Dayosisi asilimia 40 ya sadaka kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi hiyo.
Akifafanua zaidi, mtoa habari wetu alisema sharika 12 za Jimbo la Arusha Magharibi, kila moja hutoa wastani wa Sh milioni 1.8 kila wiki kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Dayosisi.
Taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili lililokuwa kanisani hapo kutoka ndani ya kikao hicho, zilibainisha kuwa Usharika wa Ngateu, ulialika wajumbe wa Halmashauri Kuu wa sharika nyingine 11 za Jimbo la Arusha Magharibi kwa ajili ya kupata msimamo wa pamoja.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, sehemu ya msimamo wa pamoja unaopangwa kuwekwa na wajumbe hao ni pamoja na kumrudisha kazini Mchungaji Philemon Mollel wa Usharika wa Ngateu aliyesimamishwa na kufukuzwa kazi baada ya kutofautiana na uongozi wa dayosisi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi za Dayosisi hiyo, Mchungaji Mollel alivuliwa uchungaji na kuachishwa kazi kwa makosa mabaya katika utumishi wake.
“Hatua hii ilichukuliwa na Dayosisi kwa mujibu wa taratibu za Kanisa …pamoja na kanuni na taratibu za Dayosisi,” ilieleza taarifa rasmi ya Dayosisi.
Hata hivyo kabla ya kuachishwa kazi, Mchungaji Mollel alishirikiana na baadhi ya waumini kupinga waraka wa Askofu uliowataka waumini wa Dayosisi hiyo wapatao 600,000 kila mmoja kuchanga Sh 20,000 ili kuzuia mali za Kanisa zisipigwe mnada.
Mali hizo ikiwemo Hoteli ya kitalii ya Corridor Springs na Hospitali ya Selian ziliwekwa rehani ili kupata mkopo wa Sh bilioni 11 kwa ajili ya hoteli hiyo, ambazo hazikurudishwa kwa wakati na kusababisha benki hiyo kutishia kuzikamata.
Katika sakata hilo, Mchungaji Mollel alitaka waliosababisha uzembe huo wawajibike kwanza kabla ya waumini kukubali kuchanga fedha kunusuru mali hizo, jambo lililotafsiriwa kuwa kosa na kusababisha aachishwe kazi.
Kuachishwa kazi kwa Mchungaji Mollel kuliibua mgogoro kati ya Usharika wa Ngateu aliokuwa akiuongoza na Dayosisi na sasa usharika huo umeanza jitihada za kuhusisha sharika nyingine za Jimbo la Arusha Magharibi kuwaunga mkono.
Katika kikao cha jana katika azimio la kuzuia sadaka kwenda dayosisi, walikubaliana sababu kubwa ni kutoona faida na miradi inayoendeshwa na Dayosisi.
Wajumbe hao wakiwemo waalikwa kutoka sharika nyingine za jimbo hilo, walidai kuwa miradi ya Dayosisi imekuwa ikinufaisha viongozi wachache wa dayosisi hiyo.
Kikao hicho pia kimeazimia kuwa msimamo huo usilegezwe mpaka Katibu Mkuu wa dayosisi, Israel ole Karyogi ajiuzulu.