WATU WAWILI WAZIKWA HAI KABURINI MBEYA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/watu-wawili-wazikwa-hai-kaburini-mbeya.html
Kamanda Diwani Athumani. |
Wakazi wawili wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba wamezikwa wakiwa hai baada ya wakazi wenzao kuwatuhumu kuwa ni wachawi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Diwani Athumani alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kuwataja waliozikwa kuwa ni Mizinara Matela na Ernest Molela.
Kamanda alisema wakazi hao walikuwa wakituhumiwa na wanakijiji wenzao kuhusika na kifo cha ndugu yao; Nongwa Molela baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Alisema baada ya maziko ya Nongwa wakazi hao wakiwamo ndugu wa marehemu waliwanyooshea vidole wawili hao wakidai kuwa ndio wauaji na kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga.
Alifafanua kuwa kabla kundi la wana ndugu hao liliwapiga wawili hao kwa marungu na mawe na kabla ya kuwaua wakawatupa kwenye kaburi lililokuwa na kuwafukia.
Baada ya kuwazika, kundi hilo lilikwenda nyumbani kwa Ernest na kuteketeza nyumba yake kwa moto.
Mpaka anazungumza na mwandishi wa habari hizi shughuli ya kufukua miili ya watu hao ilikuwa ikiendelea ili kufanyiwa uchunguzi na alifafanua kuwa baada ya uchunguzi miili hiyo itazikwa tena kila mmoja kaburi lake.
Aidha, Kamanda alisema watu wawili wanashikiliwa na inasadikiwa ndio walioongoza kundi lililotekeleza mauaji hayo, lakini hakuwataja majina kutokana na sababu alizosema ni za kiusalama.
Mwaka jana pia matukio kama hayo yalifanyika kwa usiri mkubwa lakini ikaja kubainika siku Chifu Merere wa Wasangu aliponusurika kuzikwa akiwa hai na wakazi wa kijiji cha Ruiwa wilayani Mbarali.