MNYIKA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI LEO
https://roztoday.blogspot.com/2013/02/mnyika-kuwasilisha-hoja-binafsi-bungeni.html
![]() |
| John Mnyika. |
Bunge linaendelea na Mkutano wake wa 10 ambao katika kikao cha leo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), atawasilisha hoja binafsi akitaka wabunge wajadili na kupitisha maazimo ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es Salaam.
Mnyika katika hoja yake pamoja na masuala mengine, anataka Serikali iwasilishe bungeni mpango maalumu wa kuboresha huduma za maji safi na uondoaji wa maji taka uliopitishwa Machi 2011 kwa ajili ya kuidhinishwa.
Anazungumzia kero ya mgawo wa maji na pia ongezeko kubwa la bei ya maji kwa wananchi wa kipato cha chini wanaotegemea kupata maji kutoka sekta binafsi. Kwa mujibu wake, hununua kwa madumu kwa bei ambayo ni takribani mara 15 ya bei ya mteja anayepata maji ya bomba.
Mnyika anasema pia hali ni mbaya kwenye uondoaji wa maji taka ambao ni chini ya asilimia 10 ya makazi yaliyounganishwa katika mtandao wa taka na hivyo kuleta uchafuzi wa mazingira hususan katika maeneo yasiyopimwa.
“Hata katika maeneo yaliyopimwa jijini Dar es Salaam mitandao ya maji taka haijakarabatiwa na kupanuliwa kwa wakati kwa kuzingatia ongezeko la watu suala ambalo lisipochukuliwa kwa uzito unaostahili madhara yatatokea katika siku za usoni,” alisema Mnyika.
Mnyika anataka mpango wa dharura wa kupunguza kero ya maji ulioanza kutekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Dawasa tangu 2010, uwekewe muda wa ukomo wa kukamilika.
Anataka pia Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi wa thamani ukilinganisha ufanisi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya majisafi na majitaka Dar es Salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha mkoani Pwani na taarifa ijadiliwe bungeni.
Vile vile anataka Serikali iwasilishe bungeni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali za maji safi na maji taka ili kushughulikia upungufu uliojitokeza katika utekelezaji wa sheria zilizopo na kuweka mfumo thabiti wa usimamizi wa sekta ya maji nchini.