AJARIBU KUUA KWA KUMTEGEA SUMU MWANAME KWENYE VIATU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/ajaribu-kuua-kwa-kumtegea-sumu-mwaname.html
Mtu mwenye miaka 40 amekamatwa nchini Japan kwa tuhuma za kujaribu kumuua mwanamke mmoja kwa kumwekea sumu ya tindikali ya Haidrofloriki kwenye viatu vyake.
Tatsujiro Fukasawa amekana mashitaka kwamba aliweka kemikali kwenye viatu hivyo vya mwanamke aliyekuwa akidaiwa kumnyemelea Desemba mwaka jana.
Mwanamke huyo, mfanyakazi mwenzake wa Fukasawa, alinusurika shambulio hilo, lakini amepata madhara ya kuoza katika mguu wake wa kushoto, kwa mujibu wa taarifa.
Ilidaiwa mwanaume huyo alipata sumu hiyo kutoka sehemu yake ya kazi.
Tindikali ya Haidrofloriki ni kali mno na mara kwa mara hutumika kwa kusafishia mafuta au kuyeyushia miamba isiyohitajika.
Lakini kemikali hiyo inaweza pia kutumiwa kwenye ngozi na ndani ya mishipa ya damu ya mtu kusababisha kushindwa kwa mfumo au shambulio la moyo.
Kutokana na uwezo wa tindikali ya Haidrofloriki kupenya kwenye tishu, sumu inaweza kuibuka kupitia mfichuo wa ngozi au macho, au pale inapovutwa au kumezwa.
Dalili za mfichuo kwa tindikali ya Haidrofloriki mara zote hazithibitiki papo kwa hapo sababu muunguzo hauleti maumivu mwanzoni, lakini tiba ya kitaalamu mara zote yanahitajika.