CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/cheka-taratibu_14.html
Waziri wa Mifugo kaenda kutembelea mradi wa nyuki. Mlangoni kamkuta mlinzi na baada ya kujieleza kusudio lake mlinzi akamkatalia kuingia kwa madai ni marufuku kwa yeyote kuingia muda huo. Waziri kwa hasira akasema: "Inamaana hujui mimi ni nani? Hebu tazama kitambulisho changu! Kwa shingo upande mlinzi akamfungulia mlango na waziri akaingia kwa mikogo. Baada ya dakika chache Waziri akasikika akipiga mayowe: "Mlinzi…Mlinzi njoo nyuki wananimaliza huku!" Mlinzi kwa kujiamini akajibu: "Mheshimiwa, waoneshe kitambulisho!!" Kasheshe...
