MGONJWA WA AKILI AUA WATATU, AJERUHI 10 KIGOMA

Mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo ya afya ya akili amewaua watu watatu na kujeruhi wengine 10 kwa silaha mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kijiji cha Bitale, Leganya Rashidi alimtaja mgonjwa huyo kuwa ni Staford Richard.
Mwenyekiti huyo wa Kijiji alisema kulifanyika kazi kubwa ya kumdhibiti asiendelee kuleta madhara zaidi, lakini hadi wanafanikiwa kumkamata alikuwa tayari ameshaua watu watatu na kuwajeruhi wengine 10.
Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa mtuhumiwa huyo wa mauaji alipatwa na ugonjwa wa akili akiwa kidato cha sita na amedumu nao kwa miaka zaidi ya mitano sasa, lakini hakuwa akifanya matukio ya kupiga watu hovyo kama ilivyotokea safari hii.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Dismas Kisusi alisema kuwa sambamba na kumuua bibi yake mzaa baba aliyejulikana kwa jina la Rudia Richard, pia  aliwaua Ezema Razalo na Sebastian Julius ambao aliwapiga kwa  vitu vizito na vyenye ncha kali ambavyo vilisababisha watokwe na damu nyingi na kufariki muda mfupi baadaye.
Kamanda huyo wa polisi aliwataja watu waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na Nairu Shaban (49) na  Phedil Paul (71), ambao baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo walikimbizwa kwenye zahanati ya Bitale.
Aidha Kamanda Kisusi alisema kuwa pia mtu huyo aliwajeruhi Pendo Jumbe (35), Jumbe Budio  (50), Richard Manase (60), Rith James (55), Shukrani Manase (30), Dotto Issa (24), Remmy Kagiye (08) na Seraphina Mayage (65) ambao walipata majeraha makubwa katika sehemu mbalimbali za miili yao na wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Kigoma Maweni.
Kamanda huyo wa polisi Mkoa Kigoma amesema kijana aliyesababisha mauaji hayo anashikiliwa na polisi.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item