MTALII ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME WANANE MBELE YA MUMEWE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/mtalii-abakwa-na-kundi-la-wanaume.html
![]() |
| Mtalii huyo (katikati) akiongozwa polisi wa kike kwenda hospitali kwa uchunguzi wa afya yake. |
Genge la wanaume wanane linadaiwa kumbaka mtalii mwenye miaka 39 na kumpiga mumewe kwa fimbo wakati wakiwa mapumzikoni nchini India.
Polisi walisema kwamba wanandoa hao walishambuliwa vibaya katika Jimbo la katikati ya India la Madhya Pradesh Ijumaa usiku.
Majambazi hayo yaliwashambulia wawili hao katika kijiji karibu na mji wa Datia, alisema mkuu wa polisi wa wilaya CS Solanki.
Hili ni tukio la karibuni kabisa kati ya mlolongo wa mashambulio ya ubakaji katika India ambalo limeshitua bara zima, baada ya moja la msichana mwenye miaka 23 kubakwa na kujeruhiwa Desemba, na msichana wa miaka 29 ambaye alikokotwa kwenye basi na kubakwa na kundi la wanaume sita Januari huko Amritsar.
Wanandoa hao walikuwa wakisafiri kwa kutumia baiskeli kutoka Orchha kwenda Seonda na kuamua kuweka kambi karibu na kijiji usiku huo.
Kundi la wanaume liliwavamia wanandoa hao, kuwapiga kwa fimbo kabla ya kumshinda nguvu mwanaume huyo na kuanza kumbaka mkewe, mume huyo alidai.
Polisi walisema kundi hilo kisha likaiba mali za wanandoa hao na kutokomea kusikojulikana, imeripotiwa.
D.K. Arya, mkuu msaidizi wa polisi alisema kundi hilo lilichukua kompyuta ndogo, pesa taslimu Rupia 10,000 (sawa na Pauni za Uingereza 120) na simu ya mkononi, imeripotiwa.
Mwanamke huyo kutoka Uswisi alipelekwa hospitali, ambako uchunguzi wa kitabibu ulithibitisha kwamba alikuwa amebakwa, imeripotiwa.
CS Solanki alisema watu wanane wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo, lakini maofisa bado wanaendelea kuwasaka wote waliohusika na shambulio hilo.
Katika mfululizo wa matukio ya kushitusha, mwanamke huyo aliwekwa hadharani huku wapigapicha wakihaha kumpiga picha, masaa machache baada ya kuwa ameshambuliwa.
Akiwa amefunikwa kwa taulo kuziba uso wake na kichwa, maofisa wa kike wa polisi walishika mikono ya muathirika huyo wakati wakimpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.
Picha yake ilipigwa wakati akivutwa katikati ya msitu wa watu.
Mwanamke mmoja hubakwa kila baada ya dakika 20 nchini India, kwa mujibu wa Shirika la Taifa la Kumbukumbu za Uhalifu.
Lakini polisi wanakadiria kila baada ya masaa manne matukio 10 ya ubakaji huripotiwa, kwa kiasi kikubwa kutokana na waathirika kuhofia kupata aibu kwa familia na jamii zao.
Mwanamke huyo wa Uswisi na mumewe walikuwa wakitalii jimbo hilo kwa kutumia baiskeli na waliweka kambi usiku kwenye msitu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi, Tilman Renz ameelezea tukio hilo kama 'linalosumbua akili' na kusema wanadiplomasia wa Uswisi walikuwa wakiwasaidia wanandoa hao.
Wanadiplomasia hao wamezitaka mamlaka za India 'kufanya kila kitu haraka kuwapata wahusika hivyo kuwezesha kuchukuliwa hatua," Renz alisema katika taarifa yake.
Mwezi uliopita, Serikali ya Uswisi ilitoa tangazo la usafiri kwa India lililohusisha onyo kuhusu 'kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na makosa mengine ya udhalilishaji' katika taifa hilo la Kusini mwa Asia.
Shambulio hilo limekuja takribani miezi kadhaa baada ya shambulio la kutisha dhidi ya mwanamke mmoja katika mji mkuu wa India.
Watuhumiwa sita wanasubiria huku kufuatia shambulio hilo la ubakaji dhidi ya msichana wa miaka 23 mwanafunzi wa udaktari mjini Delhi, Desemba mwaka jana.
Mmoja wa watuhumiwa amefariki baada ya kukutwa akiwa amejinyonga katika selo yake.