CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/cheka-taratibu_20.html
Jamaa mmoja kaenda kuomba kazi kwenye hifadhi ya wanyama na kujibiwa kwamba kuna uhaba wa sokwe. Hivyo jamaa akatakiwa kujifanya sokwe ili kuvutia watalii. Jamaa akakubali na kupatiwa ngozi yenye manyoya kama sokwe ili avae. Siku ya kwanza kazi jamaa akafungiwa kwenye banda na kufanikiwa mno kuwavutia watalii. Siku iliyofuata banda lake likawekwa juu ya banda lenye simba. Katika kuongeza madoido, jamaa akatoboa sakafu ya banda lake na kutumbukia kwenye banda lenye simba. Jamaa akaanza kupiga kelele: "Mama nakufa!!" Yule simba akajibu: "Acha ujinga wewe, mie mwenyewe ni binadamu kama wewe! Hebu rudi kwenye banda lako fasta kabla watalii hawajagundua!" Duh...