RAIS KIKWETE AMKUBALI PAPA FRANCIS I, ATARAJIA MAKUBWA KWAKE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/rais-kikwete-amkubali-papa-francis-i.html
![]() |
| Rais Jakaya Kikwete. |
Rais Jakaya Kikwete, ameonesha matumaini kwa Papa Francis I kwa kuchaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki Duniani na kutarajia mabadiliko makubwa.
Pia Rais amempongeza na kuahidi kuendeleza na kudumisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Vatican.
Alisema atamwandikia barua rasmi ya kumpongeza na kumtakia kila la heri na kumhakikishia ushirikiano huo ambao umedumu tangu kipindi cha Papa watakatifu waliopita akiwamo mstaafu Benedict XVI.
Rais Kikwete alitoa pongezi hizo za awali kwa Papa huyo juzi kwenye ukumbi wa Magadu mjini hapa kupitia hotuba yake baada ya kukamilika kwa harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kigurunyembe.
Kwenye harambee hiyo ambayo lengo lake lilikuwa ni kupata Sh milioni 200, Rais Kikwete alifanikisha kuvuka lengo la uchangishaji kwa kufikisha jumla kuu ya Sh milioni 255.
Kati ya hizo, zilipatikana Sh milioni 73.7 taslimu, ahadi ikiwa ni Sh 155.3 na kiasi kilichobaki ni ahadi ya vifaa vya ujenzi wa Kanisa hilo zilizotolewa na wachangiaji.
Akimzungumzia Papa Francis I, Kikwete alisema alipata kusoma habari zake, hivyo akamwelezea kuwa kiongozi anayependa masikini.
“Nimesoma habari za Papa mpya, Wakatoliki wamepata kiongozi wa aina yake, anayependa masikini, aliyetumia muda wake mwingi kwao Argentina akifanya kazi na masikini na kuwasaidia,“ alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kutaja sifa zingine za Papa kuwa ni kiongozi asiyependa maisha ya fahari na aliyekuwa akitembea kwa kutumia usafiri wa basi badala ya gari binafsi.
“Jana (juzi) baada ya kuchaguliwa kuwa Papa ilibidi aende hotelini alikofikia kuhama na hakutuma mtu,“ alisema Rais na kuongeza: “Alikwenda mwenyewe, akabeba mizigo yake na kwenda Mapokezi ya hoteli akalipa fedha na kupanda basi kurudi Vatican.”
Pia alimtaja Papa Francis I, kuwa katika historia ya Kanisa Katoliki kwani ni mtu wa aina yake na kwa matendo hayo, wananchi wa nchi masikini wana matumaini makubwa kutoka kwake.
“Kama anawajali masikini kwa kiasi hiki, ninaamini kutakuwa na sura mpya na mabadiliko mapya,“ alibashiri Rais Kikwete kwenye hotuba hiyo.
Awali, Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo la Kanisa Katoliki Morogoro, kabla ya kumkaribisha Rais kutoa hotuba yake, alimshukuru kwa kukubali ombi la kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa Kanisa hilo.
Askofu Mkude alisema Kingurunyembe ni sehemu ndogo ya Tanzania anayoiongoza, na ameamua kujishusha kwa kujali wanyonge na kutia nguvu wananchi na kudhihirisha kuwa ni kiongozi anayejali wanyonge bila kubagua.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo, kuiomba Serikali ihakikishe inalinda usalama wa watu na mali zao yakiwamo majengo ya ibada ili yasiendelee kuharibiwa kwa kuchomwa moto na viongozi wake kudhuriwa.
Alisema si jambo zuri kwa wananchi wachache kuharibu mali na majengo yanayojengwa na wananchi kwani kuendelea kufanya hivyo ni kuondoa dhana ya upendo na uelewano katika jamii na kuomba Serikali iendelee kudhibiti vitendo hivyo.
Kuhusu Papa, Askofu Mkude alimtaja kuwa kiongozi aliyetokana na watu wa chini wanaoishi maisha ya kawaida na aliyekuwa karibu na watu bila kujali uwezo wa mtu na amekuwa ni Papa wa kwanza kutoka nje ya bara la Ulaya kwa zaidi ya miaka 400 na safari hii ametoka nje ya Bara hilo - Amerika ya Kusini.