RUBANI WA NDEGE ILIYOUA WATU 228 ALIPUMZIKA KWA SAA MOJA TU...

PICHA KUBWA: Vikosi vya uokoaji vikishughulikia moja ya mabaki ya ndege hiyo baharini. PICHA NDOGO: Marc Dubois.
Rubani wa ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa ambayo ilianguka kwenye bahari na kupoteza maisha ya abiria 228 alikuwa amepumzika kwa saa moja tu kabla ya kurusha ndege hiyo, imefahamika jana.
Katika ripoti ya maapizo ambayo itawaogopesha wanaoruka angani kwa masafa marefu, inaonesha kwamba marubani wake wasaidizi pia walikuwa wamechoka mno.
Waingereza watano na Wamarekani wawili walikuwa ni miongoni mwa waliofariki wakati ndege namba AF447 ilipoanguka kutoka angani ilipokuwa safarini kutoka Rio de Janiero nchini Brazil kwenda Paris, Juni 2009.
Wakati ndege hiyo Airbus A330 ikiyumba huku na huko kwenye kimbunga cha tropiki, Pierre-Cedric Bonin - miaka 32 na David Robert - miaka 37, walishindwa kumudu kuidhibiti ndege hiyo.
Hata pale Marc Dubois - rubani mwenye miaka 58, aliporejea kutoka mapumzikoni, wasaidizi wake walikuwa wamejawa hofu kubwa kuweza kumweleza tatizo gani lilikuwa likiwakabili.
Uchambuzi wa kina wa visanduku viwili vyeusi vya kurekodi matukio ya ndege hiyo, vimeonesha kwamba vihisi mwendokasi wa ndege hiyo vilikumbwa na hitilafu - inawezekana sababu zilikuwa vimeganda barafu mno.
Lakini sasa rekodi ya Dubois imebainisha ikisema: "Sikulala vya kutosha usiku wa jana. Saa moja - haitoshi."
Le Point, jarida la habari la Ufaransa ambalo lilipata ripoti ya mahakama ambayo haikuwekwa wazi kuhusiana na janga hilo, linasema kwamba Dubois alikuwa tayari 'ananguruma' chini ya nusu saa na nusu ndani ya ndege.
Marubani hao walitumia usiku huo mjini Rio na wake zao na marafiki zao wa kike, lakini haikuonekana kuchukua tahadhari ya kutosha kukabiliana na msoto wa mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari.
Walipuuza taratibu za kawaida na kupandisha, badala ya kushusha, pua ya ndege hiyo wakati iliposhindwa kuinuka - au 'kusota'.
Msoto wa elimu ya mwendo angani haikufua dafu katika injini hizo, ambazo wachunguzi wanasema ziliendeshwa na kutumika wakati wote.
Matokeo yake ilikuwa kutumbukia kwa dakika tatu na nusu kabla ya kujikita kwenye bahari hiyo.
Wote waliokuwamo ndani - ambao walitoka katika mataifa 32, ikiwamo watano kutoka Uingereza, watatu kutoka Ireland, na wawili kutoka Marekani - walifariki baada ya ndege hiyo kujikita baharini ikiwa kwenye spidi ya futi 180 kwa sekunde.
Mamlaka ya Usalama wa Anga ya Ufaransa tayari imetoa ripoti ambayo inakubaliana na hukumu ya mahakama yenye kurasa 365 kwamba 'rubani alishindwa majukumu yake' na 'kuwazuia wasaidizi wake kuchukua uamuzi unaotakiwa'.
Majaji wa Ufaransa wamefungua mashitaka ya jinai dhidi Shirika la Ndege la Ufaransa na Airbus kwa madai ya kusababisha kifo.
Marubani wasaidizi Bonin na Robert walikuwa wamesafiri masaa 2,900 na 6,500 kwa kufuatana, kulinganisha na Dubois 11,000. Licha ya hilo, Dubois alichukua zaidi ya dakika moja kupokea simu kwa ajili ya msaada.
Wote kwenye ndege hiyo akiwamo mke wa Bonin mwenye umri wa miaka 38, Isabelle, ambaye alikuwa akisafiri bila watoto wao wawili wa kiume, wenye umri wa miaka minane na minne.
Jaji tayari ameamuru Shirika la Ndege la Ufaransa kulipa takribani Pauni za Uingereza 120,000 kama fidia kwa familia za marehemu, lakini kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka.
Shirika la Ndege la Ufaransa limepitia na kuboresha taratibu zake za mafunzo tangu kuanguka kwa ndege hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item