VATICAN YAPIGA MARUFUKU KURIPOTI MCHAKATO WA PAPA MPYA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/vatican-yapiga-marufuku-kuripoti.html
![]() |
| Makardinali wakiwa katika moja ya mikutano yao na Papa Benedict XVI. |
Vatican imepiga marufuku vyombo vya habari kuripoti mikutano inayofanywa na makadinali, wakati wa mchakato wa kumpata kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki Duniani.
Hatua hiyo imewafunga midomo viongozi wa kanisa hilo kutoka Marekani, ambao wamekuwa na utamaduni wa kuhojiwa na vyombo vya habari, mara kunapomalizika mikutano ya siri, inayoendelea katika Jiji la Vatican.
Kwa sasa makadinali wanahudhuria mkutano wa ndani, unaoandaa mkutano wa kumchagua Papa umetoa taarifa za kupiga marufuku vyombo vya habari kuripoti mkutano huo wa siri.
Marufuku hiyo ilisababisha kufutwa kwa mikutano ya kila siku na wanahabari, ambayo ilikuwa inafanywa na makadinali wa Marekani.
Gazeti la La Stampa la Italia limetaja sababu rasmi za kupigwa marufuku vyombo vya habari kuripoti tukio hilo, kwamba ni kutokana na kuwepo kwa baadhi ya taarifa za siri, zinazojadiliwa na makadinali kuhusu matatizo mbalimbali, ambayo yanalikumba kanisa hilo kwa sasa.
Lakini, habari zisizo rasmi, zimebainisha kuwa uamuzi huo ni kuwanyamazisha Wamarekani, ambao wamekuwa wanaropoka kuwepo kwa vitendo vya rushwa na vitendo vinavyoenda kinyume na matakwa ya Kanisa, vinavyofanywa katika harakati za kumpata mrithi wa Papa Benedict XVI.
Matokeo yake, kumetokea mgogoro miongoni mwa viongozi wa Kanisa hilo, wakati wanapoelekea kwenye uchaguzi huo muhimu, kwani makadinali wa Marekani na Ujerumani wanataka Papa ambaye atalegeza baadhi ya mambo, yanayofanywa katika utamaduni wa Vatican.
Lakini, makadinali wenye makazi katika Jiji la Vatican, wametaka mfumo wa sasa wa uongozi, ambao umekuwa unafuatwa na mapapa wote waliotangulia, uendelee na kusiwepo na majadiliano zaidi juu ya suala hilo.
Kadinali mstaafu, Giovanni Lajolo wa Italia alisema urasimu wa Vatican unaelekeza kuwa ni mambo mazuri tu ndiyo ambayo yanastahili kusemwa au kutangazwa.
Kadinali huyo ambaye alikuwa mtawala katika himaya ya kipapa ya Vatican, alisema wakati wa uzinduzi wa kitabu kimoja, kuwa mfumo wa uongozi ndani ya himaya hiyo unaweza kuboreshwa zaidi.
Kauli hiyo inaonesha kuwepo kwa ushahidi dhidi ya madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa, vinavyodaiwa kufanywa na makadinali, ambavyo viliripotiwa mwaka uliopita baada ya nyaraka binafsi za Papa kuanikwa na mwandishi wa habari wa Italia.
Nyaraka hizo zinaonesha kuwepo kwa mgogoro katika himaya hiyo ya kipapa iliyoko ndani ya Italia, ambayo imejaa urasimu wa upatikanaji wa habari.
Hata hivyo, Vatican imekanusha kuwepo kwa shinikizo kutoka kwa makadinali wa Marekani hadi kuwapiga marufuku kuzungumza na vyombo vya habari.
Msemaji wa Vatican, Askofu Federico Lombardi alisema mkutano maalumu wa kiroho, utafanyika wiki hii na unatakiwa kuwa siri, kwani ni moja ya mchakato wa kumchagua Papa. Pia, alikiri kuwa hakuwa anapendelea mfumo wa Marekani wa kuweka kila jambo hadharani.
"Makadinali wote wamekubaliana kwa kauli moja kuwa ni vyema wakanyamaza wakati watakapokuwa kwenye mchakato huo,” alisema.
Mjadala huo umekuja wakati Vatican inasubiri kuwasili kwa Kadinali Jean-Baptiste Pham Minh Man wa Vietnam, ambaye atakamilisha idadi ya wajumbe ambao wanatakiwa kumchagua Papa mpya.
Kadinali huyo alitarajiwa kuwasili jana Alhamisi na atakapowasili, jopo la makadinali wataanza mchakato wa kuweka tarehe ambayo itamchagua Papa. Jumla ya makadinali 115 ndio wanatarajia kumchagua papa mpya.
Jana Msemaji wa makadinali wa Marekani, Mary Ann Walsh, alisema taarifa za Kanisa hilo zilizokuwa zinatolewa na mabosi wake pamoja na mahojiano waliyokuwa wanafanya na vyombo vya habari, vimefutwa.