WIFI YAKE WHITNEY HOUSTON ANUSURIKA KUJIUA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/wifi-yake-whitney-houston-anusurika.html
Pat Houston. |
Hivi ndivyo ilivyotokea ... masaa kadhaa kabla Pat hajatuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, "Wakati fulani unaweza kujisikia kukata tamaa katika maisha na ina changamoto nyingi. Na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ... Nimechoka ...na hatimaye ninataka kupumzika. Ninawapenda sana."
Vyanzo vya habari vimeeleza wanafamilia kadhaa waliiona taarifa hiyo na haraka wakachukua hatua ... walianza kupiga simu na kumtumia meseji Pat lakini hawakujibiwa. Kisha walikwenda kwenye nyumba yake, na kukuta kalala kitandani kwake kando ya chupa iliyojaa vidonge ndani yake ... na kuamua kupiga simu ya dharura.
Imeelezwa mara polisi walipowasili, Pat aliamka na kuelezea kwamba alikuwa amekunywa tu dawa za maumivu ya mgongo, kuzima simu yake na kisha kwenda kulala -- bila kufahamu kwamba watu wengi walikuwa wakijaribu kuwasiliana naye.
Imeelezwa Pat alimtaarifu kila mmoja ... hakuwahi hata siku moja kujitoa mhanga, taarifa aliyoweka kwenye Facebook ilisababishwa na mawazo.
Vyanzo vya habari vya kisheria vimeeleza, Pat alipelekwa hospitali -- kama hatua za kumkinga -- na kuruhusiwa muda mfupi baadaye.