APIGA PICHA MZIMU KWENYE SIMU YA MKONONI BILA KUFAHAMU...


Mwanamke mmoja wa Texas amepokea mshangao wa kutishia pale alipobaini bila kufahamu amepiga picha ya mzimu kwenye simu yake ya mkononi.

Marcella Davis wa Cleveland, alikuwa akijaribu kupiga picha ya mpwa wake nje ya shule yake ndipo akageuka na kumtaka aache kumpiga picha.
Lakini baadaye, pale binti yake alipopitia picha zilizoko kwenye simu yake, alimwita mama yake kuja kutazama kivuli cha mfu kilichojitokeza nyuma kikiwa kimevalia suti ya rangi ya pinki iliyopauka ya mtindo wa miaka ya 1970.
"Kwangu, ilikuwa heshima kubwa," Marcella alieleza. "Haikuwa kitisho kwangu."
Mama huyo wa vijana wadogo wawili wa kuwazaa, Marcella anakiri hakufahamu manjonjo ya kamera ya simu yake ndio maana binti yake alimfundisha jinsi ya kuvuta kwa ukaribu picha baada ya kuwa amezipiga April 15.
Akikumbukia jioni hiyo, alisema: [Binti yangu] alisema, "Mama, angalia hii." Nilimjibu kwa dharau, "Nini?" na alinionesha picha hizo za mzimu. Ungeweza kuona moja kwa moja."
Kama haitoshi, katika kufunga uchunguzi, umbile la mwanaume aliyevalia suti.
Anayeonekana kwa mbali ni mwanamke aliyesimama kando yake.
Aliongeza: "Watu hufariki kila wakati. Hadi unapokuwa mmojawapo uliyefariki, huwezi kwa hakika kufahamu nini kilichokutokea."
Kwa wenye kushuku ambao wanaweza kumtuhumu yeye au binti yake kwa kuichezea picha hiyo kwa kutumia programu kama GhostCam, alisisitiza hakuwa hata akifahamu jinsi ya kutumia programu kama hiyo na hata kama angekuwa nayo.
"Ninaweza kukuahidi sikuitengeneza picha hiyo," anashikilia hivyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item