BI KIDUDE AFARIKI DUNIA MJINI UNGUJA...

Marehemu Bi Kidude enzi za uhai wake.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba msanii mkongwe wa muziki wa taarabu hapa nchini, Kidude Binti Baraka maarufu kama Bi Kidude amefariki dunia mchana huu.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vinavyoaminika, Bi Kidude amefariki mjini Unguja baada ya kuugua kwa muda mfupi akiwa nyumbani kwake maeneo ya Rahaleo.
Pia umri mkubwa nao unasemekana kuchangia kifo chake japo hadi mauti yakimfika alikuwa hafahamu umri wake halisi.
Bi Kidude atakumbukwa sana kwa umahiri wake wa kuimba na kucheza licha ya umri mkubwa aliokuwanao ambapo aliweza kutamba na nyimbo zake kadhaa kama Ya Laiti, Muhogo wa Jang'ombe n.k.
Kutokana na umahiri wake, Bi Kidude aliweza kupata mialiko kadhaa ya kutumbuiza katika nchi kadhaa za Ulaya ikiwamo Ujerumani.

Habari za uhakika zinasema kwamba mpaka mauti yakimfika Bi Kidude alikuwa hajabahatika kupata mtoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina. Habari zaidi endelea kuperuzi
ziro99blog.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item