MAGUFULI ASAINI MKATABA KUNUNUA KIVUKO BAGAMOYO-DAR ES SALAAM...

Dk John Magufuli.
Waziri wa Ujenzi, John Magufuli amesaini mkataba wa ununuzi wa kivuko chenye thamani ya Sh bilioni 7.9 chenye uwezo wa kubeba abiria 300 na mwendo wa kilometa 40 kwa saa kitakachokuwa kikifanya safari kati ya Bagamoyo na katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkataba huo ulisainiwa jana jijini na Waziri Magufuli kwa niaba ya Serikali na Mzabuni Mwakilishi wa Kampuni ya Johs Gram-Hanssen ya Denmark ambayo ndiyo itakayotengeneza kivuko hicho.
Kwa mujibu wa mkataba  huo, kivuko hicho kinatakiwa kukamilika ndani ya miezi minane.
Waziri Magufuli alisema kivuko hicho kimenunuliwa kwa asilimia 100 ya  fedha za Serikali kupitia Wakala wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko (Temesa) baada ya kukusanya fedha katika vivuko vingine. Kwa sasa vipo 23 nchini.
“Tumezoea kuomba misaada, lakini sasa kivuko hiki tumekinunua kwa fedha zote hakuna msaada hata kidogo, tofauti ya kivuko hiki kinaenda kwa kasi na ndani yake kitakuwa na huduma mbalimbali.
Sasa tunakwenda kumaliza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kutatua tatizo la usafiri,” alisema Magufuli.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Temesa,  Masenene Magesa alisema kivuko hicho kitakuwa na urefu wa meta 37 na upana wa meta 11 na kitakuwa na sehemu tatu tofauti za kuketi abiria huku kikiwa na migahawa ya chakula, vyoo na kitakuwa kikisimama katika vituo saba katika safari zake.
Alisema suala la msongamano wa magari Serikali imedhamiria kulitatua na ina mpango wa kununua vivuko vingine viwe jumla vitatu na pia kuboresha usafiri wa barabara na reli.
Magufuli aliipongeza Bodi ya Temesa  kwa ushauri wao wa kupandisha nauli katika vivuko kwa sababu ndiyo uliopelekea kupatikana fedha za kununulia kivuko hicho.
"Watanzania wawe wavumilivu nia ya Serikali ni kuboresha huduma lakini huduma zote zinahitaji fedha nyingi, kwa kuboresha huduma za usafiri Watanzania sasa wataamua ni njia ipi watatumia baada ya barabara kutanuliwa, vivuko kuwekwa na pia usafiri wa reli.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item