WATUHUMIWA GHOROFA LILILOANGUKA NA KUUA DAR WAPEWA DHAMANA...

Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani Kisutu, Dar es Salaam.
Watu 11 wanaokabiliwa na mashitaka ya kuua bila kukusudia watu walioangukiwa na ghorofa katika Mtaa wa Indira Gandhi, wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mfanyabiashara Razah Hussein Lazah na wenzake 10 wanaokabiliwa na mashitaka 24, waliachiwa jana.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Devotha Kisoka alitoa dhamana hiyo jana baada ya washitakiwa kutimiza masharti yaliyotolewa na mahakama.
Licha ya Lazah, washitakiwa wengine ni Diwani  katika Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed (59),  Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala,  Charles Salu (48), Mhandisi wa Majengo  wa halmashauri hiyo, Goodluck Mbaga (35) na Mkurugenzi Mkuu wa Mkaguzi wa Majengo, Willibrod Wilbard (42).
Wengine ni Mhandisi Mohamed Swaburi (61), Mhandisi Mshauri, Zonazea Oushoudada (60), Mkadiriaji Majenzi, Vedasto Nziko (59), Msanifu Majengo, Michael Hema (59), Msajili Msaidizi AQRB, Albert Mnuo na Ofisa Mkuu Mtekelezaji OQRB, Joseph Ringo.
Washitakiwa hao waliachiwa baada ya kusaini hati ya  Sh milioni 20, kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini hati ya Sh milioni 20. Pia waliwasilisha hati zao za kusafiria polisi. Hawataruhusiwa kusafiri bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Inadaiwa kuwa Machi 29, mwaka huu katika mtaa wa Indira Gandhi wilaya ya Ilala washitakiwa  waliwaua bila ya kukusudia watu 24 waliotajwa majina katika hati ya mashitaka. Kesi itatajwa Mei 15 mwaka huu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item