MWANAMKE ALIYEKIMBIA KOREA KASKAZINI ASIMULIA MATESO YAKE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/mwanamke-aliyekimbia-korea-kaskazini.html
KUSHOTO: Mto Amrok unaotenga Korea Kaskazini kutoka China. KULIA: Hyeonseo Lee. |
Mwanamke kijana ambaye alikimbia Korea Kaskazini ameibua taarifa zake za kutisha wakati akikulia kwenye taifa hilo lililotengwa, ambako alishuhudia kwa mara ya kwanza mtu akiuawa wakati alipokuwa na umri wa miaka saba tu.
Hyeonseo Lee alisafishwa kiakili kuamini kwamba nchi hiyo, inayoendeshwa na vikosi vya mauaji vya Kim, ilikuwa kubwa zaidi duniani.
Lakini alipofunguka macho yake kwenye umaskini uliopindukia na uonevu uliomzingira kila upande, alifahamu kwamba anatakiwa kutoroka, na sasa amejitenga ili kuibua hisia za kimataifa kwa ajili ya taabu za wananchi wenzake.
Lee alizungumzia kuhusu mateso yake katika mhadhara kwenye mkutano wa TED huko Long Beach, California.
Alielezea jinsi alivyokua akishawishika kwamba Korea Kaskazini ilikuwa sehemu bora kabisa kuishi huku akiimba nyimbo za kizalendo zenye vichwa kama 'Hakuna cha kuonea wivu'.
"Wakati nilipokuwa na umri wa miaka saba, niliona mauaji yangu ya kwanza hadharani - lakini nilifikiri maisha yangu katika Korea Kaskazini yalikuwa kawaida," alisema.
Haikuwa hivyo hadi 1995, wakati wa tukio la kwanza katika mfululizo wa njaa kali kuivamia nchi hiyo, ndipo kwa mara ya kwanza akagundua uzito wa taabu za raia wengi wa Korea Kaskazini.
Mama yake alipokea barua ya kushitua moyo kutoka kwa dada wa mwenzake, na kumsomea Lee.
"Utakaposoma hii, wanafamilia wote watano hawatakuwapo katika dunia hii, sababu hakuwa tumekula kwa wiki mbili zilizopita," ilisomeka barua hiyo. "Tunalala sakafuni pamoja, na miili yetu ni dhaifu mno tunasubiria kifo."
Muda mfupi baadaye, akashuhudia kitu kingine cha kushitusha nje ya stesheni ya treni - mwanamke mmoja alikuwa amelala chini akikaribia kukata roho, akiwa na mtoto mwenye njaa mikononi mwake akimtazama usoni.
"Hakuna aliyewasaidia, sababu kila mmoja alikuwa akilenga kujitunza wenyewe na familia zao," alisema Lee.
Aliamua kuchukua jukumu kubwa hatari la kutoroka kupitia Mto Amrok ambao unaigawa Korea Kaskazini kutoka China.
Wakati huo, mamia machache ya Wakorea Kaskazini walikimbia nchi hiyo kila mwaka - ingawa wengi walijaribu na kushindwa na miili yao mara kwa mara kuonekana ikielea kwenye mto huyo baada ya kushindwa kwa majaribio yao ya kutoroka.
Lee alifanikiwa kuvuka mpaka huo, akiiacha familia yake nyuma - lakini hakuwa ameiepuka kabisa hatari.
Sababu China ni mshirika wa karibu sana wa Korea Kaskazini, ikakataa kuwapa hadhi ya ukimbizi wale wote waliokimbia nchi hiyo, badala yake ikawataja kama wahamiaji haramu.
Kama Lee angekamatwa na mamlaka za China, angeweza kurejeshwa kwenye nchi yake asilia na pengine kufungwa jela au hata kuuawa.
Alitumia miaka 10 akificha utambulisho wake halisi nchini China - ingawa polisi waliwahi kumhoji kwa tuhuma za kuwa Mkorea Kaskazini kwa siri, lakini uwezo wake mkubwa wa kuzungumza Kichina ulitosha kuwahadaa.
Msaliti huyo kisha akahamia Korea Kusini, akiwasili mwaka 2008 na kupata makazi mapya na elimu ya chuo.
Hatahivyo, ingawa Korea Kusini kwa ujumla inakaribisha wakimbizi kutoka Kaskazini, uamuzi wa Lee haukuwa bila hatari baada ya mamlaka katika nchi yake ya nyumbani kuwa ikifahamika kwa kutoa adhabu kali kwa wote ambao wana ndugu Kusini.
Hivyo pale maofisa wa Korea Kaskazini walipokamata fedha alizotuma kwa familia yake, Lee alifahamu angetakiwa kuwa ameondoka haraka kuwaokoa kutoka katika janga hilo.
Akaamua kurejea Kaskazini, na kuwasindikiza katika safari ya basi ya umbali wa maili 2,000 kupitia China hadi jimbo la Laos lililoko Kusini-Mashariki mwa Asia.
Wakati gari hilo liliposimamishwa na polisi wa China, Lee alihofia mabaya, lakini aliweza kuwaokoa ndugu zake kutoka katika hatari hiyo.
"Wakati polisi huyo wa China alipoikabili familia yangu, ghafla nikasimama, na nilimweleza kwamba hawa ni watu viziwi na mabubu ambao nilikuwa nikiwachunga," alisema. "Alinitazama kwa mashaka, lakini kwa bahati aliniamini."
Familia hiyo ikafika Laos, lakini wahamiaji hao wasio salama walikuwa wamewekwa jela na maofisa walarushwa na Lee hakuweza kumudu kutoa hongo ambayo ingewezesha kuachiwa huru.
Raia mmoja wa Australia alimwona akitokwa machozi mtaani, na baada ya kuuliza tatizo lililomkumba alikwenda kwenye ATM na kutoa fedha ambazo Lee alikuwa akizihitaji.
Alipoulizwa na Lee kwanini alikuwa akimsaidia, raia huyo alijibu: "Sikusaidii wewe - Nawasaidia watu wa Korea Kaskazini."
Lee sasa anafanya kampeni kwa ajili ya kupata msaada kutoka mataifa zaidia ya kimataifa kusaidia waasi wa Korea Kaskazini na familia zao ili kusaidia ujenzi wa taifa hilo lililotengwa na dunia.
Zaidi ya miaka mitano iliyopita, wastani wa watu 2,400 wamekuwa wakikimbia nchini hiyo kila mwaka.