UTAFITI WABAINI BANGI INAFAA KUONDOA KABISA MAUMIVU MWILINI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/utafiti-wabaini-bangi-inafaa-kuondoa.html
Mmea wa bangi ukiwa shambani. |
Bangi ikiwa katika hali ya vidonge inaweza kufanya kazi vizuri kabisa kuondoa maumivu kuliko ikiwa katika hali ya moshi na kuwa na madhara kidogo mno, wamesema wataalamu.
Utafiti mpya, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York, kudhoofisha soko linalochipua la tiba ya bangi Marekani, ambalo sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.3 na linatarajiwa kufikia Dola za Marekani bilioni 9 katika miaka mitatu ijayo.
Dawa hizo za kulevya zinatumika zaidi na wagonjwa waougua saratani, kukacha kwa tishu na hali nyingine za maumivu makali.
Nchini Uingereza, Sativex, marashi ya mdomoni yaliyozalishwa kutokana na bangi, yamepatiwa leseni na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Kiafya, lakini imebaki kuwa ngumu kwa wagonjwa kuzipata kwa sababu bima nyingi za afya zimekataa kuziweka kwenye orodha zake kufuatia gharama zake kubwa.
Katika majaribio mapya kwa wanaume 30 na wanawake, baadhi walivuta dawa hiyo ya kulevya, wengine walitumia kemikali hiyo katika hali ya kidonge kinachoitwa dronabinol na waliobaki walitumia placebo, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kwenye jarida la Medical News Today.
Dronabinol inajumuisha kiambato cha tetrahydrocannabinol, kinachofahamika zaidi kama THC.
THC husaidia kukata taarifa kutoka mwisho wa mishipa ya fahamu inayofika kwenye ubongo ambayo baadaye hukomesha maumivu.
Washiriki walitakiwa kuweka mikono yao kwenye maji baridi yanayokaribia barafu na kutakiwa kuhesabu inachukua muda gani kuanza kuhisi maumivu na muda gani kila mmoja angeweza kuweka mikono yao ikiwa imezamishwa.
Matokeo yalionesha kwamba wavutaji wote na wote waliotumia vidonge waliweza kuvumilia maumivu kwa muda mrefu.
Lakini katika hali ya kushangaza, wote ambao walitumia dronabinol waliweza kustahimili maumivu kitambo kirefu zaidi kuliko wavutaji waliotumia dawa hiyo ya kulevya katika hali ya kienyeji.
Na uvutaji dawa hiyo ya kulevya kwa kitambo kulipunguza hisia za maumivu kwa masaa mawili na nusu, vidonge hivyo viliendelea kutoa athari za upunguzaji maumivu kwa zaidi ya masaa manne.
Hatahivyo, athari hizo za kutuliza maumivu za vidonge hivyo zilichukua muda mrefu zaidi kufanya kazi - dronabinol ilichukua saa moja kulinganisha na dakika 15 tu kwa kuvuta dawa hiyo ya kulevya.
Wote walioshiriki kwenye zoezi hilo pia waliripoti kwamba waligundua athari hizo za dronabinol pungufu katika kuweza kuanisi, kulinganisha na watu ambao walivuta bangi, wakisema kwamba vigonge hivyo vina uwezo mdogo katika tabia mbaya.
Bangi ya tiba ni ruksa kisheria katika mahimbo 18 nchini Marekani, na utafiti wa hivi karibuni umeonesha kwamba sehemu kubwa ya Wamarekani inaamini dawa hiyo itahalalishwa.
Utafiti uliofanywa na PewResearch Centre for People and the Press umeonesha kwamba kwa mara ya kwanza katika miaka 40 asilimia 52 ilisema kwamba inatakiwa kuhalalishwa na asilimia 72 ikisema uchukuaji huo wa sheria za kinidhamu dhidi ya dawa hizo hauendani na thamani ya fedha zinazoigharimu serikali.
Kura hiyo hiyo ilionesha kwamba karibu nusu ya Wamarekani walikiri kuwa wamejaribu bangi kwa wakati fulani maishani mwao.
Utafiti huo mpya unasema vidonge vya bangi vinaweza kutuliza maumivu kwa muda mrefu bila kuleta madhara ya kiafya ambayo yanayokuja sambamba na uvutaji," alisema mtafiti Ziva Cooper, profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Columbia.
Hatahivyo, aliongeza kwamba tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha matokeo hayo.
Kwa sababu utafiti huo ulihusisha watu wenye afya njema, haijafahamika kama wote wanaosumbuliwa na maumivu sugu wataweza kupata matokeo chanya kutokana na vidonge hivyo.
Tafiti zilizopita zimeonesha kwamba uvutaji wa bangi husaidia kupunguza maumivu kwa ujumla, maumivu katika mishipa ya fahamu, kuboresha usingizi na hali.