BAADA YA VIPIMO, MWANAUME WA MIAKA 66 AAMBIWA KUWA NI MWANAMKE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/06/baada-ya-vipimo-mwanaume-wa-miaka-66.html
![]() |
| Jiji la Hong Kong vilikofanyika vipimo vya manaume huyo. |
Mwanaume mmoja raia wa China ambaye alikwenda kwa madaktari akiwa na uvimbe tumboni ameelezwa kwamba yeye ni mwanamke.
Mtu huyo mwenye miaka 66, ambaye anazo hata ndevu, ameishi maisha yake yote kama mwanaume lakini alielezwa na madaktari huko Hong Kong kwamba kutanuka kwa utumbo wake mkubwa kulisababishwa na kuvimba kwa ovari.
Vipimo vilibainisha mgonjwa huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo mawili adimu ya vinasaba ambayo kwa muda mrefu hayakuwahi kugundulika.
Walimwonesha mgonjwa huyo alikuwa na Turner Syndrome, hali ya kinasaba ambayo huathiri takribani mmoja kati ya watoto wa kike 2,000, na kuongezeka kwa homoni za kiume.
Jarida la Kitabibu la Hong Kong, ambalo lilichapishwa taarifa hizo juzi, lilisema matukio sita tu ya watu wenye mivurugano yote waliripotiwa kwenye vituo vya matibabu.
Turner Syndrome kwa kawaida inatokana na matatizo ya programu ya kurithisha tabia na maumbile na inaweza kuwafanya wanawake kuwa wagumba na wafupi kuliko kawaida.
Wanawake wenye dalili hiyo wanakosa moja au sehemu yao ya pili X ya programu ya kurithisha tabia na maumbile.
Congenital adrenal hyperplasia huathiri moja kati ya uzazi 15,000 na kusababisha tabia za kiume kujitokeza mapema au isivyo kawaida.
Mgonjwa huyo alikua akiwa yatima na kudumaa baada ya kubalehe akiwa na umri wa miaka 10 na alikuwa na urefu wa futi 4.5 tu.
Mgonjwa huyo pia hakuwahi kufanyiwa vipimo na alikuwa na 'uume mdogo sana', kwa mujibu wa ripoti hizo.
Wasichana wenye matatizo hayo wana viungo vywa kawaida vya uzazi vywa kike lakini wanaweza kusumbuliwa na matatizo ya uzazi.
Madaktari saba, wakiandika kwenye jarida hilo, walisema mgonjwa huyo mzaliwa wa Vietnam anaweza kuendelea kuishi kama mwanaume na pengine kubadilishwa testosterone.
