HUKUMU YA UPATU WA DECI KUTOLEWA JULAI 26
https://roztoday.blogspot.com/2013/06/hukumu-ya-upatu-wa-deci-kutolewa-julai.html
![]() |
| Baadhi ya wanachama wa DECI wakiwa wamekusanyika nje ya makao makuu ya ofisi za DECI, Mabibo, Dar es Salaam mara baada ya serikali kutangaza kufungwa ofisi hizo. |
Hukumu ya kesi ya kuendesha na kusimamia mchezo wa upatu (DECI) inayowakabili vigogo wa taasisi hiyo inatarajia kutolewa Julai 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Mkazi Hellen Riwa atatoa hukumu hiyo baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na majuisho ya hoja yaliyowasilishwa kwa njia ya maandishi.
Kesi hiyo inawakabili wachungaji wa makanisa tofauti ya Pentekoste, ambao ni Jackson Mtares, Dominic Mtares, Timotheo Ole Loitingye na Arbogast Francis.
Julai 17, mwaka jana Mahakama hiyo, iliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu na kuwataka kujitetea baada ya mashahidi 16 wa upande wa mashitaka, kutoa ushahidi wao.
Washitakiwa wanadaiwa kati ya mwaka 2007 na Machi 2009 katika Makao Makuu ya Deci, Mabibo Dar es Salaam walikusanya fedha kutoka kwa wananchi wakiwaahidi kuwa watapata faida ya riba kubwa, katika mpango huo waliouita kupanda na kuvuna pia walifanya shughuli hiyo bila leseni.
Wanadaiwa kuchukua amana za watu bila ya kibali kwa kuwa waliomba kibali cha kuendesha shughuli za kifedha na si cha kuchukua amana na katika utetezi wake Mchungaji Mtares alikiri kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliwakataza kupokea fedha kutoka kwa mwanachama yeyote wa taasisi hiyo .
Inadaiwa kuwa zaidi ya Watanzania 700,000 nchini walijiunga na taasisi hiyo na walikuwa wakipanda na kuvuna pesa.