MBUNGE NASSARI ASIMULIA MKONG'OTO ALIOPATA...

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa kitandani hospitalini.
Akielezea kupigwa kwake, Mbunge Joshua Nassari akizungumza na Mbowe  na Nyalandu hospitalini hapo,  alisema alikuwa kwenye kata yake ya uchaguzi lakini ghafla alizingirwa na watu zaidi ya 30.

Alisema katika kundi pia walikuwamo watu watatu wenye asili ya Kisomali  ambao wawili kati yao ni wakazi wa jimbo lake la Arumeru.
“Walinishambulia  na kunipiga  hali iliyonilazimu kukimbilia kwenye gari langu  na kutoa bastola ili kujihami, lakini wakati nakimbia  nilizidiwa nguvu na watu hao na kuamua kukimbia sehemu asiyoijua ili kuokoa uhai wangu,” aliongeza Mbunge huyo.
“Hivi siasa kwa kweli tunakwenda pabaya maana mtu anashambuliwa bila sababu, nimeumizwa mimi pamoja na mawakala na viongozi wa Chadema waliokuwa Makuyuni,” alisema. 

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item