MTOTO WA MFLAME ALISHITAKI JARIDA LA FORBES KWA KUPUNGUZA UTAJIRI WAKE...

Prince Alwaleed bin Talal.
Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia analishitaki jarida la Forbes kwa upotoshaji sababu lilimtaja kuwa ana utajiri wenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 20 tu katika orodha ya jarida hilo ya utajiri inayochapishwa kila mwaka badala ya Dola za Kimarekani bilioni 30.

Prince Alwaleed bin Talal, mmoja wa wafanyabiashara matajiri zaidi duniani, anadai jarida hilo lilishusha utajiri wake kwa Pauni za Uingereza bilioni 9 pale lilipomuweka katika nafasi ya 26 kwenye orodha yake ya mwaka huu.
Kwa kuorodheshwa kama mwenye utajiri wenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 29 kungeweza kumuweka katika orodha hiyo kati ya kumi bora.
Alwaleed alilishutumu Forbes, kwa upendeleo dhidi ya wawekezaji wa Mashariki ya Kati na taasisi zao za fedha katika mahojiano na gazeti la Sunday Telegraph mwezi Machi, mwaka huu.
Mtoto huyo wa Mfalme sasa amechukua hatua ya upotoshaji dhidi ya mchapishaji wa jarida hilo Randall Lane na waandishi wawili katika Mahakama Kuu mjini London, imeripotiwa.
Atadai kwamba Orodha ya Utajiri imeharibu hadhi yake na mapato ya kampuni yake ya Kingdom Holdings.
Kampuni yake ya Kingdon Holdings inaendesha vitegauchumi ikiwamo hisa katika Apple, Facebook, Twitter na Shirika la Habari la Rupert Murdoch.
Mali zake zinajumuisha Hotel ya Savoy, Plaza mjini New York, mlolongo wa Hoteli za Four Seasons na hisa za umiliki wa jengo la Canal Wharf la London.
Forbes lilikokotoa utajiri wa Mtoto huyo wa Mfalme kwa kuzingatia thamani ya vitegauchumi vyake vinavyofahamika badala ya bei ya hisa katika Taduwal, Soko la Hisa la Saudi Arabia, lilisema.
Mtoto huyo wa Mfalme alisema: "Sifanyi kwa sababu ya utajiri wangu, lakini sababu wanaishutumu Saudi Arabia kwa kuwa haina makasino. Hii haikubaliki."
Msemaji wa Forbes alieleza: "Tumeshangazwa mno kuhusu madai kwamba Prince Alwaleed ameamua kulishitaki Forbes, hasa kama amefanya hivyo ndani ya Uingereza."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item