MWANAUME ADAI KUISHI MIAKA MITANO BILA KULA CHAKULA...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/mwanaume-adai-kuishi-miaka-mitano-bila.html
![]() |
Kirby de Lanerolle. |
Mwanaume mmoja nchini Sri Lanka anadai ameweza kuishi bila kula chakula kwa miaka mitano iliyopita.
Ingawa wataalamu wanaamini wanadamu wanaweza tu kuishi kwa miezi miwili bila kula, Kirby de Lanerolle anasisitiza alikuwa akihitaji tu hewa safi kama kirutubisho.
Ingawa wataalamu wanaamini wanadamu wanaweza tu kuishi kwa miezi miwili bila kula, Kirby de Lanerolle anasisitiza alikuwa akihitaji tu hewa safi kama kirutubisho.
Mtu huyo pia anadai mtindo wake wa maisha - ambao anasema hufanya kazi ya kawaida kwenye mwanga, upepo na 'mirindimo ya Mungu' - unaweza kurudisha nyuma umri na kumfanya aishi milele.
Katika mahojiano ya kipindi cha televisheni cha Taboo USA kinachonaswa na The Sun, de Lanerolle alisema: "Kuna vyanzo vya nishati hapo ambavyo ni vikubwa kuliko kalori za chakula unazoweka katika mwili wako.
"Kalori zinakuja kutoka kwenye fotoni na mwanga na mirindimo na upepo. Kila kitu kinaweza kukulisha kama vyanzo vyako vya nishati viko wazi."
Anakiri kuwahi kula milo saba yenye kalori 500 katika kipindi cha zaidi ya miezi kumi iliyopita, lakini anadai ilimfanya ajihisi mgonjwa.
Alisema: "Katika utambuzi huu, pale ninapokula chakula, inanifanya nijihisi mchovu mno. Na hisia zangu zinatoweka pale ninapokula sasa."
Kwa mujibu wa tovuti moja, de Lanerolle alikuwa muathirika wa dawa za kulevya akiwa na umri wa miaka 16.
Lakini aliendelea na kuwa mshindi wa medali ya Dhahabu katika Ubingwa Ulengaji Shabaha kwa bunduki aina ya Rifle ngazi ya Taifa kwa Vijana mwaka 1995, mshindi wa medali kadhaa za ndondi, Mshauri Mkuu wa Wizara ya Huduma za Jamii nchini Sri Lanka na mfanyabiashara mwenye mafanikio.
Pia anaaminika kuwa mtu pekee anayefahamika kumaliza marathoni akiwa ametumia maji pekee kwa miezi mitatu.
Ndani ya miaka mitano iliyopita, alisoma kuhusu watu ambao hawakula chakula hadi kufikia miaka sita na kutokunywa maji hadi kufikia siku 40 na usiku 40.
Pia alivutiwa na machapisho ya gwiji aliyesema kwamba saratani, kisukari na maradhi ya moyo yanasababishwa na chakula.
Sasa anataka kuwafundisha wengine kuwa watu wanaokula hewa, lakini wataalamu wanahofia kuhusu madai yake sababu baadhi ya watu wamekufa wakijaribu kuiga mtindo wake huo wa maisha.