SASA NJIA NYEUPE KWA PAPA JOHN PAUL KUTANGAZWA KUWA MTAKATIFU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/07/sasa-njia-nyeupe-kwa-papa-john-paul.html
Papa Francis jana amewapitisha mapapa wawili wenye mvuto zaidi katika karne ya 20 kuwa watakatifu, akithibitisha muujiza unaohitajika kumtakatifuza Papa John Paul II na kupitisha sheria za Vatican kumtunukia Papa John XXIII.
Katika kuthibitisha mamlaka yake ya kipapa, Francis aliamua kwamba John XXVIII anaweza kutambulika mtakatifu hata kama Vatican haijathibitisha muujiza wake wa pili aliofanya wakati wa kipindi chake. Vatican ilisema Francis alikuwa na nguvu ya kuachana na mahitaji hayo na kuendelea na moja pekee lililothibitisha muujiza kwa jina lake.
Sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Desemba 8 imetajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kufanyika sherehe hizo.
Maaskofu wa Poland wameendelea kushinikiza iwe Oktoba, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 35 ya kuchaguliwa kwa mzaliwa huyo wa Poland, John Paul, lakini maofisa wa Vatican wamesema kwamba ni mapema mno kuandaa tukio kubwa kama hilo.
