NDEGE YAGEUZA NA KUREJEA UWANJA KUMCHUKUA BINTI WA MIAKA 11 ALIYEACHWA...

Ndege hiyo baada ya kurejea uwanjani hapo.
Ndege ya shirika la ndege la Israeli - kwa msaada wa kila mmoja kwenye ndege hiyo - iligeuza ilikotoka kwenda kumchukua mgonjwa wa saratani mwenye umri wa miaka 11.
Mgonjwa huyo aliyekamilisha mipango yote kwenda New York Agosti 7 kuhudhuria kambi ya watoto wagonjwa wa saratani, Inbar Chomsky, alishushwa kwenye ndege ya El-Al Airlines baada ya pasipoti yake kupotea. Licha ya msako mkali uliofanywa na mfanyakazi wa shiriki hilo la ndege, abiria na kundi ambalo Chomsky alikuwa akisafiri nalo, pasipoti yake haikuweza kupatikana, wahudumu wa kwenye ndege hawakuwa na jinsi ila kumshusha msichana huyo mgonjwa.
Huku wakibubujikwa na machozi, kila mmoja akampungia mkono msichana huyo aliyepagawa baada ya msako wa nusu saa akisaidiwa na wafanyakazi wa ndege hiyo na abiria ukishindwa kuipata pasipoti ya msichana huyo, kwa mujibu wa taarifa.
"El-Al kwa huzuni ilimpigia simu mama yake kumtaarifu kwamba pasipoti ya Inbar ilikuwa imepotea na kwamba msichana huyo, ambaye alikuwa akipambana na maradhi kijasiri mno, hatoweza kusafiri kwenda Camp Simcha's Rabbi Yaakov Pinsky, mkurugenzi wa tawi la Chai Lifeline nchini Israeli aliandika kwenye Yeshiva World News: "Mateso gani haya aliyopitia msichana wa miaka 11."
Dakika kadhaa baada ya milango kufungwa na ndege kuondoka kwenye lango hilo, mwenzake mmoja alimtazama nyuma ya mzigo wa msichana mwingine na kuiona pasipoti ya Chamsky na kuwaeleza wahudumu wa ndege, kwa mujibu wa Haaretz.
Marubani wa ndege hiyo haraka wakasimamisha ndege hiyo, kwa mujibu wa Haaretz, na baada ya takribani dakika 45 waliweza kuwashawishi waongozaji ndege kuwaruhusu warejee kwenye lango hilo kumchukua Chomsky, aliandika Pinsky.
Akiwa bado anajaribu kurejea kawaida kutokana na kuchanganyikiwa wakati bado akiwa kwenye lango hilo na Elad Maimon, meneja programu wa tawi la Chai Lifeline nchini Israeli, Chomsky na wengine walitazama bila kuamini ndege ikigeuza na kurejea, ilisema Haaretz.
"Wahudumu wa ndege hawakuweza kuamini macho yao," Maimon alilieleza gazeti hilo. "Walinieleza kamwe hawakuwahi kuona kitu kama hicho."
"Mara chache mno ndege huwa zinarejea kwenye lango baada ya kuondoka, ilisomeka taarifa ya El-Al, ikaendelea kwamba "baada ya kushauriana na mfanyakazi wa El-Al kwenye ndege uamuzi ukafikiwa na ndege hiyo ikarejea kumchukua Inbar."
"Abiria walipongezana na kulia, aliandika Pinsky, akisema walishiriki 'furaha na taharuki ya Inbar', na kuiita 'moja ya matukio makubwa kabisa' ambayo hakuwahi kushuhudia."

Related

WorldNews 2022706917649597216

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item