EAC yatakiwa kuimarisha sekta ya nishati

BENKI ya Maendeleo Afrika (AfDB) imezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuimarisha ushirikiano wao katika sekta ya nishati. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kanda wa AfDB, Gabriel Negatu, wakati akitoa ufafanuzi na kusema kwamba hatua hiyo itavutia soko kubwa la wawekezaji katika kanda hiyo.

“Kutakuwa na upatikanaji wa fedha zaidi katika kanda iwapo kutakuwepo na miradi ya maana,’’ alisema Negatu.

Hivi sasa nchi za EAC zinakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa nishati ya kutosha na hivyo kufanya kanda hiyo ya kiuchumi kushindwa kushindana ipasavyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB), kanda ya Afrika Mashariki ni eneo lenye uchumi unaokua kwa kasi duniani.

Viwango vya uzalishaji umeme kwa nchi nyingine za EAC na kiwango kwenye mabano ni pamoja na Kenya (megawati 1700), Uganda (megawati 680), Rwanda (megawati 110).

Na Ronald Ndungi, EANA

Source @Mtanzania

Related

Science 7328492391368656513

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item