ALIYEIGIZA NA SCHWARZENEGGER ADAI TALAKA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/03/aliyeigiza-na-schwarzenegger-adai-talaka.html
Mwigizaji Penelope Ann Miller ambaye ameigiza kama Doris kwenye filamu ya "The Artist" amewasilisha kortini maombi ya kutaka kutengana na mumewe, imefahamika rasmi.
Miller mwenye miaka 48, aliwasilisha maombi hayo kwenye Mahakama Kuu ya Los Angeles wiki iliyopita. Mwigizaji huyo amewahi pia kucheza kama mpinzani wa Arnold Schwarzenegger kwenye filamu ya "Kindergarten Cop."
Miller na mumewe, James Huggins walifunga ndoa mwaka 2000 na kufanikiwa kupata watoto wawili.
Moja ya vituko vyake visivyoweza kusahaulika ni pale alipoolewa na mwigizaji mwenzake Will Arnett katika ndoa iliyodumu kwa mwaka mmoja tu kuanzia mwaka 1994-1995.
