BOBBI KRISTINA AUFYATA KWA BIBI YAKE...

Katika hali inayoonesha kama kuufyata mkia, binti 'mtukutu' wa gwiji wa zamani wa muziki Hayati Whitney Houston ameibuka na kukanusha uvumi na tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwake hasa kwenye mahusiano yake ya mapenzi.
Bobbi Kristina mwenye miaka 19, amekanusha vikali habari kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na kaka yake wa kufikia, Nick Gordon baada ya kuonekana hadharani akiwa amevalia pete ya uchumba ambayo imedaiwa amevikwa na Nick.
Bibi yake Bobbi, Cissy Houston amekuwa akikemea vikali mahusiano hayo kwa kuuita urafiki huo ‘haramu’.
Lakini msemaji wa ‘mtukutu’ huyo ameueleza mtandao wa MailOnline jana kuwa binti huyo pekee wa Whitney Houston hajachumbiwa na kwamba pete anayovaa ni ya marehemu mama yake.
“Bobbi Kristina hajachumbiwa. Anavaa tu pete ya mama yake,” alisema msemaji huyo.
Ukanushaji huo umekuja siku nne baada ya wawakilishi wa Bobbi kuhojiwa na MailOnline baada ya ripoti kuzagaa kwamba yeye na Nick wamepanga kuoana, ripoti ambazo wawakilishi hao walishindwa kusema chochote juu ya madai hayo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao walionekana wakiwa sambamba matembezini na Alhamisi iliyopita Bobbi Kristina alionekana akianika pete hadharani wakati akibusiana na Nick.
Katika sehemu ya wosia ulioachwa na Whitney Houston, Bobbi Kristina amerithishwa vito vyote vya thamani ikiwamo pete inayozusha mkanganyiko.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item