ADAI MUNGU KAMTUMA AMCHINJE BOSI WAKE...
https://roztoday.blogspot.com/2012/03/adai-mungu-kamtuma-amchinje-bosi-wake.html
PICHA KUBWA: Geti la Hoteli ambako mauaji ya Varian yalifanyika. PICHA NDOGO JUU KUSHOTO: Chris Varian. PICHA NDOGO JUU KATIKATI: Jonathan Limani. PICHA KULIA: Jonathan Limani akiwa na pingu mara baada ya kukamatwa.
Mhamiaji kutoka Albania ambaye alimchinja Meneja wa Mgahawa mmoja, Chris Varian, kwa kutumia kisu cha kukatia jibini ameruhusiwa kwenda Uingereza licha ya kufanya vurugu na vitendo vyake vya ukichaa alivyofanya barani Ualaya kwa miaka mitano.
Jonathan Limani, ambaye ameainishwa kama 'mtu hatari sana', alilazimika kuhojiwa faragha mara mbili na amekuwa akichunguzwa kutokana na vitendo vyake vya udhalilishaji wakati aliporuhusiwa kuhamia Uingereza.
Familia ya Varian, ilisema juzi kuwa mamlaka zimetoa 'mtiririko wa dosari' zilizoibuka kumruhusu Limani kuhama Sweden na kuwa mhudumu kwenye Hoteli ya Nyota Nne ya The Oxfordshire, mjini Thame.
Limani mwenye miaka 34, alikana mashitaka lakini alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kwa sababu ya kupunguziwa majukumu kwenye Mahakama ya Oxford Crown, juzi.
Limani ambaye amekuwa akifanya kazi hotelini hapo usiku tu, alimuua bosi wake kwa kile kilichoelezwa 'Sauti ya Mungu' imemuagiza kufanya hivyo, alieleza daktari wa magonjwa ya akili mahakamani hapo.
Varian ambaye wakati huo alikuwa na miaka 32, alitoka na kwenda mapumziko mafupi kwenye eneo la kuvutia sigara.
Limani akachukua kisu cha kukatia jibini na kumfuata kwa nyuma kumpiga kabla hajatenganisha kichwa na kiwiliwili.
Mwendesha mashitaka, Alan Blake alisema, "Mpishi Guy Hathaway-Pearce alishuhudia mtuhumiwa akiwa amepiga magoti huku kashika shingo ya Varian." Hali ya Varian ilikuwa mbaya sana na Limani alikuwa akimtazama kikatili.
Tukio hilo utenganishaji kichwa lilichukua 'muda na nguvu', uchunguzi ulibainisha.
Limani alitiwa hatiani kwa kuua bila kukusudiam huku upande wa mashitaka ukikubali hoja kwamba alikuwa hana akili timamu wakati akitekeleza dhamira yake hiyo ya kuua.
Limani amewahi kuchunguzwa mara mbili na kupatiwa matibabu ya ukichaa nchini Sweden na Uswisi. Alikuwa akipatiwa tiba mara kwa mara. Mwaka 2004 amewahi kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.
Pia amekuwa akichunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji nchini Uswisi ambapo aliomba hifadhi ya ukimbizi alipohamia Uingereza.
Baba wa Varian, Nigel alisema juzi kwamba kifo cha kijana wake kimekuwa kikiichoma familia kila siku. Ametaka kujua kwanini mtuhumiwa amekubaliwa kuingia nchini.
"Muuaji amekuwa na historia ya matukio ya ukichaa kwa zaidi ya miaka mitano. Tunatumaini Serikali italichukulia kwa umakini tukio hili. Kuna kila dalili za tukio kama hili kujirudia," alisema Nigel.
Jaji Anthony King amesema Limani amekuwa ni 'mtu hatari sana.'
Akitoa hukumu ya kifungo cha miaka isiyopungua 19, Jaji King alisema mauaji ya Varian yalikuwa ni tukio la 'shambulio baya zaidi la kudhuru mwili.'
Kabla ya kuswekwa jela, Limani atapelekwa kwanza kwenye hospitali maalumu kwa uangalizi na matibabu ya akili. Matatizo yake hayo ya akili yakipungua ndipo ataanza kutumikia kifungo.
Idara ya Usalama wa Ndani ya Nchi imesema Limani hakuwamo kwenye orodha yake ya watu hatari wakati alipopewa ruhusa ya kuhamia Uingereza.
Polisi waligundua mwili wa Varian kwenye viwanja vya mchezo wa gofu eneo ambako Limani alikuwa akishinda. Mtuhumiwa alikamatwa eneo la tukio.
Limani, ambaye alikuwa na wiki tatu tu tangu aingie Uingereza kabla ya kumchinja Varian, alifahamika kwa jina la kichaa, akiwa amekamatwa mara mbili kutokana na matatizo ya akili nchini Sweden.
Chini ya kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuja Uingereza, muuaji huyo anadaiwa kujaribu kumpora bunduki askari polisi. Alikamatwa kwa kosa hilo.
