CHEKA TARATIBU...

Daktari mmoja aliamua kufanya ziara ya kawaida kuwatembelea wagonjwa wake wa akili wodini. Alipoingia tu wodini akamkuta mgonjwa wa kwanza akiwa ameketi sakafuni huku akiigiza kukata kipande cha mbao. Mgonjwa wa pili alikuwa akining'inia kichwa chini miguu juu darini. Daktari akamuuliza mgonjwa wa kwanza anafanya nini darini. Mgonjwa wa kwanza akajibu, "We huoni kuwa hapa nakata mbao?" Daktari akamuuliza tena mwenzake anafanya nini pale juu. Mgonjwa wa kwanza akajibu, "Ooh huyo ni chizi kidogo. Anafikiri yeye ni balbu." Daktari akatazama juu na kugundua jamaa kama anaungua. Basi daktari akamwambia mgonjwa wa kwanza, " Kama ni rafiki yako, unatakiwa kumtoa pale kabla hajadhurika." Hapo hapo mgonjwa wa kwanza akafoka, "We mjinga nini, nimtoe halafu nifanye hii kazi gizani?" Mh...

Post a Comment

  1. Jamani mbavu zangu mie. Mnavitoa wapi hivi vichekesho. Yani nimetembele blogu nyingi lakini hapa ndio sibanduki, a lot of materials.

    ReplyDelete

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item