CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/03/cheka-taratibu_22.html
Jamaa kaenda kwa dokta na kusema, "Dokta, nina matatizo.Kila mara nilalapo kitandani nahisi kuna mtu kajificha uvunguni. Ninapohamia uvunguni nahisi kuna mtu juu ya kitanda. Basi usiku kucha ni juu chini juu chini. Naomba msaada wako maana naelekea kupata wazimu." Dokta akajibu, "Njoo kwangu mara tatu kwa wiki, nitakutibu hofu yako." Jamaa akauliza, "Utanichaji kiasi gani?" Dokta akajibu, "Elfu moja kila ukija." Baada ya miezi sita kupita dokta akakutana na jamaa mitaani. Dokta akauliza, "Mbona hukurudi tena?" Jamaa akajibu, "Kwa elfu tano tu mhudumu wa baa kanitibu." Dokta akahoji, "Kivipi?" Jamaa akajibu, "Kaniambia nikakate miguu ya kitanda."
