MFUASI WA AL QAEDA AUA, AJIUA UFARANSA...


Huyu ndiye kijana Mohammad Merah ambaye ameuawa kwenye mapigano ya kutupiana risasi na askari nchini Ufaransa jana. Imeelezwa kwamba kwanza alijificha bafuni baada ya kugundua kuwa amezingirwa na askari. Akatoka ghafla na kuanza kumimina risasi kama njugu na kujeruhi maofisa wawili wa polisi, huku mmoja hali yake ikiwa mbaya. Hatua ya kumvamia kwenye jengo lake imekuja baada ya vitisho kwamba amepanga kuwaua polisi. Kabla ya kukimbilia Ufaransa, Merah alitoroka gerezani nchini Afghanistan mwaka 2008 na tangu wakati huo amekuwa akisakwa kwa udi na uvumba. Wakati akizingirwa, ndani alikuwa na silaha mbalimbali zikiwamo bunduki aina ya SMG, Kalashnikov, Riffle na silaha nyingine. Askari watatu wamejeruhiwa vibaya wakati wakijaribu kumtia nguvuni. ziro99blog itawaletea mkasa mzima ambao ulikuwa mithili ya filamu pamoja na video! Endelea kuperuzi...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item