CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/03/cheka-taratibu_2861.html
Mkaguzi anaendesha gari kuzunguka shamba usiku. Wakati anaendelea kukagua uzio wa shamba hilo akasikia kishindo kwa nje. Akachukua simu yake na kumpigia bosi wake, “Bosi nimepata tatizo huku, nimemgonga nguruwe na kanasa kwenye ngao ya gari huku akiendelea kukoroma. Nifanyeje?” Bosi akajibu, “Nyuma ya kiti kuna bunduki, mpige risasi ya kichwa kisha mkokote ukamtupe kichakani.” Jamaa akajibu, “Sawa bosi.” Baada ya dakika kumi akapiga tena simu, “Bosi nimefanya kama ulivyosema, nimemtwanga risasi ya kichwa na kumtupa kichakani.” Bosi kwa ukali akajibu, “Sasa tatizo nini tena?” Jamaa akasema, “Taa za bluu kwenye pikipiki yake bado zinawaka!” Duh, ujinga kweli kazi…
