BARUA YA MICHAEL JACKSON KUELEZA KINACHOMSIBU YAANIKWA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/05/barua-ya-michael-jackson-kueleza.html
Barua ya Michael Jackson aliyoandika kwenda kwa Lisa Marie Presley akilalamika kuhusu tatizo ambalo pengine ndilo lililosababisha kifo cha Mfalme huyo wa Pop Duniani imetua rasmi mezani mwa kampuni ya mnada.
Lisa Marie hakusema kwanini anataka barua hiyo inadiwe, lakini ni dhahiri kwamba Michael alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kukosa usingizi kwa miaka mpaka alipopata suluhisho la haraka kwa kutumia dawa aina ya Propofol.
Barua hiyo iliyoandikwa kati ya mwaka 1993 na 1996, inasomeka kama ifuatavyo: "Nusa hapa (mshale ukielekeza kwenye kisanduku). Lisa nahitaji kwa dhati mapumziko. Sijapata usingizi kwa siku nne sasa. Nahitaji kuwa mbali na simu na wafanyabiashara. Lazima nichukue tahadhari kuhusu afya yangu kwanza, napagawa kwa ajili ya penzi lako."
Julien' Auction ya mjini Beverly Hills, kampuni ileile iliyouza Nyaraka za siri za Elvis Presley imekabidhi kwa hiari kwa binti wa Elvis.
Mmiliki wa kampuni hiyo, Darren Julien ameeleza, "Nafikiri ni kitu binafsi, na tulitaka kuheshimu ombi na kuendeleza mahusiano mazuri na Lisa."
