MARY J. BLIGE AJUTIA 'MADUDU' YA TAASISI YAKE...


Mary J. Blige amejifunza somo muhimu kuhusu kujitolea tangu taasisi yake iliposhitakiwa kwa kushindwa kurejesha mkopo wa Dola za Marekani 250,000 akieleza kuwa alifanya makosa kuiacha huru na kusababisha ufujaji mkubwa wa fedha na kwamba sasa analipa kwa makosa yake.
Imevujishwa kwamba, Mary J. Blige and Steve Stoute Foundation for the Advancement of Women Now (FFAWN)inashitakiwa na Benki ya TD kwa kushindwa kurejesha mkopo wa Dola za Marekani 250,000 iliyochukua Juni, 2011.
Benki ya TD inadai kuikopesha FFAWN pesa Juni, 2011 na FFAWN ilikubali kulipa ifikapo Desemba, 2011, lakini mpaka sasa, benki hiyo imepokea kiasi cha Dola za Marekani 368.33 tu.
Sasa, Mary amesema, "Kama mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa FFAWN, nawajibika kwa kila kitu kilichokwenda hovyo. Tatizo ni kwamba sikuwa na watu sahihi katika maeneo mwafaka ili kufanya vitu sahihi. Hii haikutakiwa kuruhusiwa kutokea, lakini imetokea na sasa tunarekebisha."
Mwimbaji huyo amesema anafanya kazi bila kuchoka na timu yake mpya ya wataalamu 'kuirejesha Taasisi hiyo kwenye mstari, kulipa madeni mbalimbali na na kusimamia kikamilifu majukumu ya FFAWNS.'

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item