CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/05/cheka-taratibu_30.html
Baada ya kazi ngumu za siku hiyo mwili ukiwa umejipumzisha ndipo viungo vikaanza malumbano kwa kila kimoja kudai kina majukumu mazito kuzidi vingine. Baada ya kila kimoja kutaja ugumu wa majukumu yake ikaonekana vyote viko sawa kwa uzito wa majukumu yao. Wakati kila kimoja kikiamini hivyo, ndipo makalio yakaongezea, "Pamoja na umuhimu wangu wote, lakini mimi ndio ninatandikwa viboko bila hatia kwa makosa ama ujinga wa watoto majumbani na mashuleni!" Duh...
