NGUO ZILIZOPOTEA CHUMBANI KWA WHITNEY ZAPATIKANA...

Aliyekuwa mpenzi wa Whitney Houston, Ray J.
Saa chache kabla ya mbunifu wa mavazi kumshitaki mwimbaji Ray J kufuatia nguo za mbunifu huyo kupotea kwenye chumba alimofia Whitney Houston Februari, mwaka huu, imeelezwa kuwa mwimbaji huyo ameziona.
Iliripotiwa masaa kadhaa yaliyopita kwamba Ray J amefunguliwa mashitaka na mbunifu wa mavazi wa Los Angeles, Marc Littlejohn, ambaya anadai alimkodisha Ray J mavazi mbalimbali yenye thamani ya Dola za Marekani 2,880 kwa ajili ya Tuzo za Grammy, na kwamba alikuwa hakuzirejesha.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, waliziacha chumbani kwenye Hoteli ya Beverly Hills ambako Whitney alifariki na tangu hapo hazikuonekana tena.
Lakini sasa mwakilishi wa Ray J amesema utata huo umekwisha tangu jana usiku pale mmoja wa washirika wa Whitney alipokabidhi nguo hizo kwa Ray J.
Vyanzo vimesema vitu hivyo vilitolewa kwenye chumba cha Whitney pamoja na vitu vingine vya marehemu. Imeelezwa watu hao wa Whitney walishindwa kumpata Ray J kutokana na mwimbaji huyo kubadili namba yake ya simu.
Vitu hivyo vilivyokuwa vimepotea ni pamoja na suti mbili na jaketi moja.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item