JUSTIN BIEBER AFANYA KUFURU NORWAY...
https://roztoday.blogspot.com/2012/05/justin-bieber-afanya-kufuru-norway.html
Bieber amepanga kucheza nyimbo zake mpya nne usiku wa kuamkia leo mjini Oslo ikiwa ni sehemu ya kipindi chake maalumu cha televisheni "Around the World" na imeelezwa mashabiki waliopagawa wa Justin kutoka bara lote la Ulaya wamevavia jiji hilo kwa ajili ya kushuhudia onesho hilo.
Imeelezwa umati ulifurika kupita kiasi kwa ajili ya kumpokea Bieber, kiasi cha polisi kushindwa kabisa kudhibiti na hivyo kulazimika kumuomba mwimbaji huyo kuanza kutumbuiza mapema kabla mambo hayajaharibika.
Kwa kufahamu kuhusu hali hiyo, Bieber alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema, "...ili onesho lifanyike kila mmoja lazima wafuate maagizo ya polisi. Wote tunahusika kwa usalama wenu na ninataka kuwapatia kile kilicho bora kwenu. Tafadhali sikilizeni."
Kwa sasa Bieber yuko kwenye sehemu ya faragha na atatua kwa helikopta jukwaani.