TYLER PERRY AKANUSHA KUKIMBIWA NA BINTI WA WHITNEY HOUSTON...

Tyler Perry amekanusha vikali ripoti zilizozagaa kuwa binti wa Whitney Houston, Bobbi Kristina ameingia mitini kuandaa Onesho lake la Televisheni "For Better Or Worse" akiziita tetesi hizo kuwa 'hazina ukweli wowote.'
Bobbi Kristina ana nafasi ndogo ya kucheza kwenye onesho hilo, lakini taarifa zimekuwa zikizunguka kwamba amejiondoa kabla ya msimu kuanza, huku akimwaga machozi wakati wa maandalizi.
Sasa Tyler, mbunifu wa shoo hiyo ametumia tovuti yake kukanusha tetesi hizo akiandika, "Hakuna uwezekano wowote wa yeye kutoka sababu tumeshamaliza zoezi la upigaji picha."
Tyler ameandika, "Kulikuwa na wakati mgumu kwake? Ndio. Si kwa sababu ya kuigiza au kazi yoyote inayofanana na hilo lakini sababu ya ukweli kwamba ndio ametoka kufiwa na mama yake."
Aliongeza, "Hivyo ndio alikuwa akisononeka, lakini alisononeka pembeni, ila alimudu kumaliza majukumu yake na alifanya kazi nzuri kwa wakati huo huo."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item