"JIRANI KUTOKA KUZIMU" AKABILIWA NA ADHABU YA KIFO...

Mwanamke mmoja raia wa Uingereza ambaye anakabiliwa na adhabu ya kifo kwa kukamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1.6 amebatizwa jina la 'Jirani kutoka Kuzimu' katika mji wa Bali.
Mama wa nyumbani Lindsay Sandiford mwenye miaka 56, anatuhumiwa kukamatwa na kilo 4.7 za cocaine Daraja A zilizofichwa kwenye sanduku lake dogo wakati akiwasili kwenye kisiwa hico cha Indonesia.
Mama huyo wa watoto wawili amefahamika kwamba anaishi Redcar mjini Cleveland, lakini kabla alikuwa mpangaji kwenye jumba moja mjini Cheltenham, Glos ambako alikuwa akilipa kodi ya Pauni za Uingereza 275,000.
Juzi, majirani zake walielezea jinsi walivyokuwa wakimchukulia kama mama anayeheshimika, lakini kumbe alikuwa jirani hatari sana.
Mzee mmoja mwenye miaka 63 anayeishi mlango unaofuatia kutoka kwa mama huyo amesema alitimuliwa nyumbani hapo takribani miaka mitano iliyopita akidaiwa kushindwa kulipa kodi ya pango.
Alisema: "Alileta hisia kwamba ni mwanamke mstaarabu, lakini kumbe hakuwa hivyo kabisa. Hakika alikuwa ni jirani kutoka kuzimu."
Mwanaume huyo alidai, kulikuwa na pilika za wanaume kuingia na kutoka nyumbani kwa mama huyo wakati wote wa usiku, na polisi walikuwa wakimtembelea mara kwa mara sababu alikuwa na utata wa kupeleka watoto wake wawili shuleni.
Aliongeza: "Haikunishangaza hata kidogo kwamba amekamatwa kwa dawa za kulevya. Sifahamu kinachoendelea kwa kweli.
"Nyumba yake ilitaifishwa kutokana na kushindwa kurejesha fedha alizokopa kutoka kwa mtu mmoja. Ninachoweza kukumbuka ni kwamba walifunga sehemu hiyo."
Alisema pia kuwa polisi walifika nyumbani hapo mara kadhaa kwa matukio tofauti.
Jirani mwenzake Colin Richardson, naye pia alikuwa mwenye furaha kuona mama huyo akiondoka hapo.
Alisema: "Nina furaha kuona akiondoka. Hakuwa mtu sahihi kwa yeye kuishi hapa kama jirani."
Sandiford alikamatwa baada ya kuingia nchini humo akitokea Bangkok akiwa na dawa za kulevya alizozipanga ndani ya sanduku lake dogo, kwa mujibu wa polisi.
Mwanamke mwingine wa Uingereza na mumewe, pia mwanaume mwingine raia wa Uingereza na mmoja mwenye uraia wa India walikamatwa baadaye baada ya Sandiford kuripotiwa walikubaliana kusuka mpango huo.
Amefahamika kuchukua nafasi kubwa katika mpango wa 'makabidhiano' kwenye sehemu ambayo haijafahamika katika kisiwa hicho cha maraha.
Polisi wa Bali juzi waliwapanga mstari watuhumiwa wote watano katika mikutano miwili tofauti na waandishi wa habari kwenye mji mkuu wa nchi hiyo wa Denpasar.
Sandiford ambaye anadaiwa kukamatwa na kilo 4.7 za dawa za kulevya aina ya cocaine, alijifunika kichwani na kuonekana akijifuta jasho wakati wakiwa ameketi uwanjani hapo.
Alivalia fulana ya gharama rangi ya njano huku akiwa kavalia miwani na vito vya thani.
Ofisa Forodha Made Wijaya aliwaambia waandishi kwamba muonekano wa upole wa Sandiford ulikuwa wa kuigiza tu.
"Licha ya mnavyomshuhudia, tunaamini kuwa amekuwa sehemu ya mtandao wa kimataifa wa biashara ya dawa za kulevya kwa muda mrefu', alisema.
"Huuni mtandao mkubwa wa kimataifa." Mzigo huo ulikatwa kwa kisu wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuonesha dawa hizo za kulevya.
Watuhumiwa wengine wanne walioneshwa wakati tofauti na polisi. Hatahivyo, sura zao zilizibwa kwa mifuko maalumu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item