"UKIMWI MPYA WA WAMAREKANI" SASA WATISHIA AMANI...

https://roztoday.blogspot.com/2012/05/mpya-wa-wamarekani-sasa-watishia-amani.html
KUSHOTO: Mzee ambaye anaaminika alileta ugonjwa huo katika Marekani miaka ya 1920. KULIA: Mdudu aina ya kombamwiko asiye na mabawa ambaye hueneza ugonjwa huo kwa njia ya damu.
Maradhi yasiyofahamika sana yanayotishia maisha ambayo husababishwa na mdudu anayefyonza damu , wataalamu wameyabandika jina la 'Ukimwi mpya wa Wamarekani.'Maradhi hayo yanayoenezwa na vimelea yanajulikana kama Ugonjwa wa Chagas yanashabihiana na hatua za mwanzo za usambaaji wa virusi vya ukimwi, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Ukiwa unafanana na Ukimwi, Chagas ni vigumu kuhisi na inaweza kuchukua miaka kwa dalili zake kujitokeza, kwa mujibu wa wataalamu walioandika kwenye Jarida la PLOS Neglected Tropical Diseases.
Ugonjwa huo ambao unapatikana zaidi Amerika ya Kusini, umesabaa Marekani kufuatia ongezeko la wasafiri na wahamiaji.
Kufuatia kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huo, idadi ya watu walioathirika na uwezo wa kujikinga, Chagas inaaminika kuwa ni moja ya Magonjwa Hatari yaenezwayo na Vimelea, kundi la magonjwa matano yanayoenezwa na vimelea ambayo yamelengwa katika mpango wa CDC kwa ajili ya utekelezaji wa afya ya jamii.
Chagas huwashambulia zaidi watu waishio katika maeneo yaliyotopea kwa umaskini na hasa taarifa za maambukizi Marekani zimekutwa kwa wahamiaji.
Kama ukiwahiwa katika hatua za awali, ugonjwa huo unaweza kukingika ndani ya miezi mitatu kwa tiba madhubuti ya vidonge,
Hata hivyo kutokana na dalili zake kutojitokeza mapema na gharama za tiba yake, Chagas imekuwa ikishindikana kutibika.
Pia una sifa ya kuenea kirahisi kupitia zoezi la kuongezewa damu na mara chache kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Benki zote za damu katika Marekani na Amerika ya Kusini wamekuwa wakichunguza damu kuona uwezekanao wa kuwako ugonjwa huo.
Benki nyingi za damu Marekani zilianza kuchunguza uwepo wa ugonjwa huo mwaka 2007.
Chagas kwa kawaida huenezwa kutokana na kung'atwa na mdudu anayekula damu aitwaye Triatome ambaye huacha vijidudu viitwavyo Trypanosoma cruzi kwenye mfumo wa damu wa mhusika.
Jamii hiyo ya wadudu hujumuisha Triatomids, kombwamwiko wasiokuwa na mabawa wenye urefu wa milimita 20 maarufu kama 'kombamwiko wanaobusu'. Jamaa zao wa karibu ni Mbung'o wanaopatikana Afrika, ambao hueneza ugonjwa wa Homa ya Malale.