MKE AHISI DAWA ZA KULEVYA SABABU ZA KIFO CHA JOHNNY TAPIA...


Mke wa bingwa wa zamani wa ndondi duniani, Johnny Tapia anaamini mumewe alitumia dawa zilizopigwa marufuku kisheria wiki moja kabla ya kifo chake, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kisheria.
Katika nakala ya maelezo ya polisi yaliyochukuliwa muda mfupi baada ya kugundulika mwili wa Tapia nyumbani kwake New Mexico wiki iliyopita na kwa mujibu wa nyaraka, mashaka hayo ya Teresa yametokana na tatizo sugu alilokuwanalo mumewe la matumizi ya dawa za kulevya. Teresa amekiri kutokuwa na vidhibiti kuongezea nguvu madai yake hayo.
Polisi hawakukuta ushahidi wowote wa dawa zilizokatazwa kisheria kwenye nyumba ya Tapia, lakini wakakuta kasha lililofungwa likiwa limejaa dawa mbalimbali za tiba zikiwamo Hydrocodone (generic Vicodin) na Quetiapine (dawa zinazotumika kutibu maradhi ya akili).
Askari wamesema wamekuta pia vidonge vya Hydrocodone kando ya mwili wa Tapia.
Wanafamilia wamewaeleza polisi kwamba Tapia alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo masaa kadhaa kabla ya kifo chake.
Uchunguzi wa kifo cha Tapia ulikamilika jana. Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kutangazwa wiki kadhaa zijazo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item