ALIYEKUWA DAKTARI WA MICHAEL JACKSON AHISI KUFA-KUFA JELA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/aliyekuwa-daktari-wa-michael-jackson.html
Dk. Conrad Murray ameungana na bondia Floyd Mayweather Jr. kumwomba jaji kutoa amri ya kumhamisha kutoka Mahabusu ya Los Angeles sababu inammaliza kabisa mwili wake na kama hatosaidia kumuondoa mapema, Murray anaamini atafia humo.
Lakini kuna kitu cha kipuuzi, tofauti na Mayweather, Murray haombi kutumikia kifungo hicho nyumbani (sababu anafahamu haitatokea)... Murray anaomba kupelekwa Gerezani, ambako anaamini atapata huduma nzuri zaidi.
Wakili wa Murray amesema, mteja wake anataka kutumikia muda wake kwenye chumba kikubwa sababu amekuwa akichukuliwa kama takataka Jela ya Los Angeles huku akipata hewa safi mara moja kwa mwezi na kubadili chupi mara moja kwa wiki.
Kutokana na madai hayo ya kunyimwa, imeelezwa afya ya Murray imeshindikana...nywele zake, kucha na ngozi vina manundunundu. Pia amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa katika wiki chache zilizopita.
Murray, ambaye alikuwa daktari wa Michael Jackson na ambaye anashitakiwa kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha Mfalme huyo wa Pop, amesema hajawahi kusumbuliwa na maradhi ya kichwa hapo kabla na anahofia inaweza kuwa ni uvimbe kwenye ubongo.
Imeelezwa kwamba Murray aliomba kuonana na daktari, lakini amekuwa akizungushwa na hajapata matibabu yoyote hadi sasa.
Murray alimweleza Wakili wake,Valerie Wass, "Siwezi kutoka hapa nikiwa hai. Hii ni sehemu ya hatari sana. Nipo hapa nakufa. Utaratibu una dhamira ya kuniua."
Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Polisi wa Los Angeles ameeleza kuwa Idara hiyo haitolei maoni yoyote kwenye kesi zilizo mahakamani.