ALIYETAFUNWA SURA SASA APATA NAFUU...

JUU: Poppo akiongozwa na wafanyakazi wa hospitali kufanya mazoezi ya kutembea kwa mara ya kwanza tangu ashambuliwe. PICHA NDOGO: Poppo kabla na baada ya shambulio na kulia ni Eugene.
Mwanaume asiye na makazi ambaye asilimia 80 ya uso wake imeliwa katika tukio la kutisha kando ya barabara kuu yenye pilika ya Miami, sasa 'ameamka na kutoa ishara', kwa mujibu wa madaktari wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Jackson ya Ryder Trauma Center.
Picha iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana zimemuonesha Ronald Poppo akitembea kwenye bwalo la hospitali, huku akisaidiwa na wafanyakazi pembeni yake.
Mtu huyo alinyofolewa jicho lake la kushoto lakini madaktari wanamatumaini ya kurejesha uono katika jicho lake la kulia ambalo limejeruhiwa sehemu kubwa katika shambulio hilo.
"Anafarijika kuwaambia wote kwamba anajisikia vizuri, anakula, anatembea kuzunguka maeneo hayo sambamba na mtaalamu wake wa viungo, anatembea na sisi," alisema Nicholas Namias, daktari wa upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Miami.
Picha hiyo imetolewa na hospitali kuonesha theluthi mbili ya sura ya Poppo imefunikwa na vigaga.
Amepoteza pua yake na matundu yake yote ya macho yamefunikwa, moja kwa kitambaa chembamba na moja kwa kile kinachoonekana kama imepandikizwa ngozi.
Ndevu zake za kijivu zimenyolewa na kubakisha mustachi juu ya mdomo wake wa juu.
Madaktari hospitalini wamesema mtu huyo asiye na makazi pia ana tundu kifuani mwake ambalo inawezekana ni la risasi iliyopigwa na ofisa wa polisi ambaye alimuua mtu aliyekuwa akimshambulia.
Nicholas Namias, mkuu wa magonjwa yanayosababishwa na kiwewe, na daktari wa Popp, alisema kwamba Poppo alikuwa na matundu mawili ya 'ajabu' kifuani mwake.
Madaktari waliongeza kwamba muathirika alipoteza jicho lake la kushoto lakini wanajaribu kuokoa jicho lake la kulia ambalo limejeruhiwa sehemu kubwa.
Poppo pia alijeruhiwa ubongo katika shambulio hilo, kama vile mtu aliyepata ajali ya gari, imeripotiwa.
Licha ya matatizo haya, timu ya madaktari imesema Poppo, ambaye amekuwa hospitalini tangu wakati wa shambulio Mei 26, anatia matumaini.
Amezungumzia kuhusu kuogelea, kitu ambacho imekuwa starehe yake kubwa, na aliagizia pizza, juisi ya machungwa na chakula cha Kitaliano.
Aliomba kuzimwa televisheni chumbani kwake, isipokuwa pale timu ya mpira wa kikapu ya Miami Heat inapocheza mechi, alisema Namias.
Daktari alisema Poppo hajawahi kuacha kulalamika maumivu yake.
"Hakika amekuwa ni mtindo tu wa maisha kwa sasa na kutaka kuongelea kuhusu vitu vya kawaida," alisema
Poppo atafanyiwa upandikizaji ngozi kadhaa kujenga upya sura yake.
Wafanyakazi wa jamii watamsaidia kutafuta sehemu ya kuishi baada ya kuwa hana makazi kwa karibu miaka 30.
Mfuko umeanzishwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Jackson kusaidia Poppo kupata Dola za Marekani 15,000. Poppo pia anafuzu kupatiwa matibabu kupitia bima za afya za Medicaid na Medicare.
"Ikiwa kama hatoweza kuona tena hapo itakuwa, anahangaika kuhusu anafananaje au zaidi kuhusu dunia inamtazamaje? Vyote ni vitu vya kuvifikiria," alisema mtaalamu wa upandikizaji sura bandia Wrood Kassira.
"Nimeongea naye kuhusu ukarabati na amesema tutafanya kitu kimoja kwa siku moja. Ni mtu anayejali sana utaratibu."
Poppo amekuwa hospitali ya Kumbukumbu ya Jackson tangu aliposhambuliwa na Rudy Eugene Mei 26, mwaka huu.
Katika shambulio hilo la kutisha ambalo limetikisa Bara zima la Amerika, Eugene mwenye miaka 31 ambaye asili yake ni kutoka Haiti, alitafuna bonge la nyama kutoka kwenye uso wa Poppo.
Moja ya picha za video za tukio hilo lililodumu kwa takribani dakika 20, watu kadhaa wanaonekana wakipatiza na baiskeli zao bila kufanya juhudi zozote kuzuia.
Taarifa zimekuja baada ya rafiki wa kike wa Eugene kuanika hadharani jina na sura yake kwa mara ya kwanza jana.
Yovanka Bryant mwenye miaka 27, aliendelea kudai mpenzi wake huyo waliyedumu naye kwa miezi minne sasa alikuwa mtulivu na mkristo mcha Mungu.
Alienda mbali zaidi kwenye madai yake kwa kusema kwamba Eugene angeweza kuwa 'baba mwema wa watoto wake."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item