WEZI WAVUNJA NYUMBANI KWA KANYE WEST...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/wezi-wavunja-nyumbani-kwa-kanye-west.html
Imeelezwa kwamba mwimbaji Kanye West sasa ni muathirika, baada ya nyumba yake ya jijini Los Angeles kuvunjwa na wezi.
Mtu mmoja kutoka kambi ya Kanye ambaye alikuwa nyumbani kwa Kanye alitoa taarifa kwa Idara ya Polisi ya Los Angeles jana asubuhi kuripoti kuvunjwa kwa nyumba hiyo. Haijafahamika kwanini, ama chochote kimechukuliwa lakini watu waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa na uthibitisho wezi hao kudondosha baadhi ya vitu vya Kanye wakati walipokuwa wakitoka ndani.
Kanye hauwapo mjini humo. Kwa sasa yuko mjini Birmingham, Uingereza akiwa katika nusu tu ya ziara yake ya matamasha.
Polisi wa Los Angeles wanachunguza tukio hilo.