ALIYEUA MWANAFUNZI KWA KUMCHOMA VISU AKAMATWA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/aliyeua-mwanafunzi-kwa-kumchoma-visu.html
Mwanafunzi wa kike mwenye miaka 15 amechomwa visu hadi kufa juzi usiku wakati wa sherehe na mvulana mmoja ambaye wazazi wake waliondoka nyumbani kwa ajili ya mapumziko.
Jana, mvulana huyo mwenye miaka 19 alikuwa akihojiwa na polisi kwa tuhuma za mauaji.
Majirani zake huko Ampthill, mjini Beds wamemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Megan-Leigh Peat mwenye miaka 15.
Alikutwa amekufa baada ya huduma za dharura kupokea simu ya 999 ikisema alikuwa 'amejeruhiwa vibaya' majira ya kuelekea asubuhi.
Majirani wamesema, mvulana huyo alikimbia nyumbani baada ya tukio hilo la kuua. Iliaminika kuwa alikuwa ametapakaa damu na kujeruhiwa kidole katika shambulio hilo la kisu dhidi ya msichana.
Jana wapelelezi walikuwa wakijaribu kila njia kuwasaka wazazi wa kijana huyo, ambao walikuwa mbali na nyumbani kwa mapumziko wakati shambulio hilo likitokea, huku wakimwacha huru kijana wao kuwaalika marafiki zake nyumbani hapo.
Madaktari wasio na mipaka na polisi walifika eneo la tukio la mauaji Barabara uya Ailesbury, eneo la Ampthill, mjini Bedfordshire muda mfupi baada ya saa 7:30 usiku.
Dakika chache tu kabla polisi walimpita mtu mmoja mtaa wa jirani ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya moja ya vidole vyake.
Madaktari hawakuweza kuokoa maisha ya msichana lakini polisi baadaye walimkamata kijana huyo kwa tuhuma za mauaji. Anaaminika alikuwa amehifadhiwa mtaa wa jirani wa Dunstable, Ampthill.
Mwanamke mmoja wa makamo anayeishi jirani na eneo la tukio ambaye hakutaka kutajwa jina alisema aliamka asubuhi na kukuta damu imetapakaa kwenye magurudumu ya gari lake la bluu aina ya Vauxhall Astra.
Alisema: "Jirani yangu ambaye anaifahamu familia inayohusika alisema kwamba msichana wa miaka 15 amechomwa visu.
"Wazazi wa kijana kwa sasa hawako nyumbani kwa mapumziko. Nimesikia kwamba kulikuwa na vijana kadhaa nyumbani hapo na kwamba kabla ya hapo walikuwa baa ya White Hart wakivuta bangi.
"Ikafika wakati fulani walilazimika kurudi nyumbani na hapo ndipo tukio hili likatokea.
"Nadhani damu kwenye gari langu imetokea kwa kijana wakati alipokuwa akijaribu kutoroka," alisema.
Jirani mwingine ambaye hakutaka kutaja jina alisema: "Familia hiyo ilihamia hapo miezi minne iliyopita. Ni wanandoa wenye miaka kama 40 na kijana wao, ambaye naweza kusema ana umri wa miaka kumi na kitu hivi.
"Walionekana kama watu wa kawaida watulivu. Nilikuwa nikimwona kijana nje akihudumia bustani.
"Mume wangu alisikia kitu jana usiku, lakini haikuwa kawaida sababu wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na sherehe kadhaa nyumbani hapo.
"Sifahamu kama kijana huyo anafanya kazi au anasoma lakini nimekuwa nikimuona anazurura na mbwa wake," alisema.
Mamlaka jana zimemtambua kijana huyo kama Megan-Leigh Peat, mwanafunzi kutoka Shule ya Harlington Upper iliyoko Dunstable, mjini Beds.
Kijana huyo amekuwa akishikiliwa na polisi rumande lakini hatarajiwi kuhojiwa na wapelelezi hadi hapo baadaye.