CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/cheka-taratibu_10.html
Jamaa alikuwa akitembea kwenye kijiji kimoja akakuta mtoto akichezea kinyesi cha ng'ombe. Kwa mshangao jamaa akauliza, "We mtoto unafanya nini hapo?" Mtoto akajibu, "Natengeneza sanamu ya Rais." Jamaa akahoji tena, "Rais? Kwanini usijaribu kutengeneza sanamu ya Mbunge wako?" Mtoto kwa uhakika akajibu, "Kinyesi hiki hakitoshi kutengeneza sanamu ya Mbunge!" Mh, noma...