ASIMULIA ALIVYOUA WATOTO WAKE WAWILI AKIHOFIA KUNYANG'ANYWA...

KUSHOTO: Lianne akiwa chini ya ulinzi mahakamani. KULIA: Rebecca (juu) na Daniel enzi za uhai wao.
Chumba cha mahakama Hispania kilikuwa kimya juzi wakati Mama wa Kiingereza alivyoelezea kwa ufasaha jinsi alivyowaua watoto wake wawili baada ya kuwafanyia mapumziko 'halisi' ya ufukweni.
Katika mahojiano na polisi kwa njia ya video, Lianne Smith alionesha jinsi alivyotumia mfuko wa plastiki unaotumika kubebea bidhaa kumziba pumzi Rebecca mwenye miaka mitano, na Daniel mwenye miezi 11 kwenye vitanda vya hoteli walimokuwa wamepanga huko Costa Brava.
Wakati Daniel akihangaika kupumua alivuta mfuko kuzingira shingo yake na 'hakuacha kukaza' hadi alipofariki, Mahakama ya Jimbo la Girona iliyoko Kaskazini-Mashariki kwa Hispania ilielezwa.
Kisha akafanya kama hivyo kwa binti yake kabla ya kuwakumbatia watoto wake na kukesha usiku mzima kando ya miili yao.
Alisema alijaribu kujiua mwenyewe kabla ya kumweleza mtu wa mapokezi hotelini hapo kuwataarifu polisi.
Mahojiano hayo yaliyorekodiwa na maofisa hao Mei 2010 kwenye chumba kinachofuatia kutoka kile ambamo mauaji hayo yalifanyika masaa kadhaa kabla yamewekwa hadharani kwa mara ya kwanza juzi.
Lianne, mwenye miaka 45 kutoka Lichfield, Staffordshire, hakuonesha kujutia wakati baraza la wazee wa mahakama wakitazama.
Alisema alichofanya na kurejea tukio zima kwa uhakika: "Nilisitisha maisha ya wanangu wawili. Kisha nikalala kitandani kando ya miili yao, niliwakumbatia.
"Niliwaongelesha hadi karibu Saa 3:00 kisha nikaenda bafuni." Kwa kutumia mikono yake, alionesha jinsi mifuko ilivyoziba midomo na pua za vijana hao.
Lianne, meneja wa zamani katika Idara ya Huduma za Watoto ya Halmashauri ya Cumbria, alifafanua jinsi alivyomuua Daniel kwanza, akisema: Nilimvalisha mfuko kichwani kwake.
"Kichwa chote kilikuwa ndani. [Nilijua atakapokuwa amekufa] sababu nilikuwa nimemshikilia.
Alipoulizwa kama binti yake alihangaika, Lianne alijibu kirahisi: "Alijisogeza, ndio."
Lianne kisha alitumia usiku huo katika chumba cha hoteli hiyo akiwa na watoto wake waliokufa akiandika mlolongo wa maandishi.
Kwa Rebecca na Daniel alisema: "Nawapenda sana. Nilitaka kuwapa maisha ya upendo pamoja. Samahani sana."
Wanaume wanane na wanawake watatu wa baraza walimkodolea Lianne lakini hata mara moja yeye hakuweza kuwatazama machoni, akaamua kutazama sakafu ya chumba cha mahakama.
Lianne anadai aliwaua watt wake sababu alihofia angenyang'anywa na Idara ya Huduma za Jamii baada ya mpenzi wake, Fundi wa Televisheni, Martin Smith ambaye hakufunga naye ndoa alikamatwa kwa madai ya kufanya ngono na mtoto.
Wawili hao walienda Hispania Desemba 2007 lakini Mei 2010, Martin Smith alikamatwa na kurejeshwa kujibu mashitaka nchini Uingereza.
Akiwa ameshinikizwa na wazo kwamba Huduma za Jamii watakuja kuwachukua watoto wake, Lianne alisema aliwahamishia kwenye hoteli ya Miramar mjini Lloret de Mar ambako alikuwa akilipia Pauni za Uingereza 53 kwa usiku mmoja.
Alianza kulia baada ya kuwaeleza polisi: "Niliwapatia wanangu mapumziko ya siku tatu, mapumziko ya uhakika. Walikuwa na furaha, walifurahi sana.
"[Lakini] ulikuwa mwisho wao. Nilijua watawarudisha watoto wangu Uingereza."
"Nilifahamu haikuwa sahihi kuondoa uhai wa mwingine. Nilihisi niko njiapanda. Dhamira yangu ilikuwa kwamba watoto wangu na mimi tungeondoka. Haikuwa watoto pekee."
Baraza la Mahakama lazima liamue kama Lianne anahusika moja kwa moja na vifo hivyo.
Mwendesha mashitaka Victor Pillado Quintas alitaka Lianne afungwe miaka 38 jela, akiwaeleza wazee wa baraza kuwa watoto 'walikuwa hawawezi kabisa kujitetea wenyewe".
Alisema: "Ikifahamika kikamilifu kwamba kutokana na umri wao mdogo na tabia yake ya kushangaza isingewezekana kwao kujitetea, tena wakati wakiwa wamelala, na kutumia mwanya wa imani waliyokuwa nayo watoto kwa mama yao, alimbeba mtoto wa kiume mkononi na kumvalisha mfuko kichwani, kuziba pande zote kuzunguka shingo yake.
"Hakuacha kukaza kwa nguvu mfuko huo hadi alipomuua. Bila kuchelewa alifanya hivyo kwa binti yake wa miaka mitano, kumziba kwa mfuko uleule kuzunguka shingo na kukaza kwa nguvu hadi binti huyo alipokufa.
"Baada ya kusitisha maisha ya watoto wake alitumia usiku huo kukaa na miili yao."
Martin Smith alishitakiwa kwa tuhuma za kumbaka kwa kurudia rudia binti wa Lianne, Sarah Richardson ambaye alimzaa kwenye mahusiano ya awali na mtu mwingine, wakati akiwa mtoto.
Sarah kwa sasa ana miaka 24 akificha utambulisho wake baada ya Martin kuhukumiwa kifungo mwaka jana mjini Manchester. Alijinyonga mwenyewe gerezani Januari mwaka huu.
Martin Smith, ambaye ni mwenyeji wa North Shields aliwahi kuwa mwimbaji kwenye bendi katika klabu mbalimbali katika North East kabla ya kujishughulisha na ufundi wa televisheni.
Wawili hao walianza kuishi pamoja mjini Cumbria na mwaka 2007 wakahamia Lichfield, Staffordshire, lakini waliishi hapo kwa miezi kadhaa tu kabla ya kwenda Hispania na Rebecca.
Daniel alizaliwa nchini Hispania Juni 2009. Mahakama juzi ilielezwa kwamba haijafahamika bayana baba wa Rebecca na Daniel. Kesi inaendelea.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item